Makamishna 4 'waasi' wa IEBC wataja sababu za kupinga matokeo

Cherera alisema hesabu za matokeo ya mwisho ya kura za urais hazikuingiana.

Muhtasari

• Cherera walitoa sababu nne za kujitenga na matokeo yalioashiria kuwa William Ruto ndiye rais mteule.

•Pia walisema matokeo ya urais yalitangazwa bila matokeo kutoka kwa baadhi ya maeneo bunge.

Makamishna Juliana Cherera, Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyangaya.
Makamishna Juliana Cherera, Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyangaya.
Image: FREDRICK OMONDI

Makamishna wanne wa IEBC ambao walipinga matokeo ya urais yaliyotolewa Jumanne wamefafanua sababu zao za

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, wanne hao wakiongozwa na naibu mwenyekiti wa tume Juliana Cherera walitoa sababu nne za kujitenga na matokeo yalioashiria kuwa William Ruto ndiye rais mteule.

Cherera alisema hesabu ya mwisho ya matokeo ya kura za urais zilizopigwa Agosti 9 haikuingiana na  ilipinga mantiki.

"Yale mahesabu hayaingiani. Sote tulienda shule. Tukiangalia katika jumla ya kura zote halali, asilimia 0.01 inatafsiri kuwa kura 142,000. Hizo ni kura nyingi sana ambazo zinaweza kubadili matokeo," Cherera alisema.

Naibu mwenyekiti huyo pia aliibua madai kuwa matokeo ya mwisho ya urais katika fomu 34C hayakuonyesha idadi ya watu ambao walipiga kura, kura halali zilizopigwa na kura ambazo zilikataliwa.

Alisema tume ilikosa uwazi kuhusu jinsi mchakato wa mwisho wa kujumlisha ulikuwa ukiendelea.

"Mchakato ambao uliingia katika kizazi cha fomu 34c haukuwa wazi," Alisema.

Aidha makamishna hao walisema walikataa kumiliki matokeo kwa sababu matokeo yanatangaza idadi ya wapiga kura waliojiandikisha, kura zilizopigwa na idadi ya kura zilizokataliwa. Hili, walisema ni kinyume cha Katiba na sheria.

"Isipoonyeshwa vinginevyo, sote tunajua kwamba asilimia hiyo inawakilisha sehemu ya idadi nzima. Kwa mfano kura halali milioni 7.17 zilizopigwa kumuunga mkono mgombea aliyeshinda zilitafsiriwa hadi asilimia 50.49 basi ilikuwa 50.49 ya nini?" Cherera alihoji.

Walihoji jinsi mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alivyosema kwamba Raila alipata asilimia 25 ya kura katika kaunti 34 huku Ruto akipata asilimia 25 katika kaunti 39 ilhali kuna kaunti 47 pekee nchini.

"Swali ni kwamba ni takwimu zipi kati ya 34 na 39 mtawalia ziliunda kigezo huru ili kuhalalisha asilimia 25 katika kaunti 34 na asilimia 25 katika asilimia 39 ya Raila na Ruto mtawalia," Cherera alisema.

Maafisa hao walisema sababu zilizotajwa hapo juu ziliarifu uamuzi wao wa kupinga matokeo.

Huku wakirejelea kesi ya Maina Kiai, makamishna hao walitaja matokeo yaliyotangazwa na Chebukati kuwa batili wakisema korti kesi hiyo ilihitimisha kuwa sheria haimpi mwenyekiti wa bodi ya uchaguzi mamlaka makubwa na yasiyo na kikomo.

Walisema sheria inawataka makamishna wote saba kuidhinisha matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa urais ili yaweze kuaminika.