EPRA yatangaza kushuka kwa bei ya mafuta

Bei hizo mpya zitaanza kutumika kuanzia Oktoba 14 saa sita usiku kwa muda wa mwezi mmoja.

Muhtasari
  • Bei hizo ni pamoja na asilimia 8 ya ushuru wa Ongezeko la Thamani ya bidhaa (VAT)
Mhudumu akiweka gari Mafuta ya petroli
Mhudumu akiweka gari Mafuta ya petroli
Image: MAKTABA

Mamlaka ya Udhibiti wa kawi na mafuta nchini imetangaza bei mpya za mafuta.

Bei ya lita moja ya petroli ya Super ilipunguzwa hadi Ksh178 kutoka Ksh179.30.

Dizeli sasa itauzwa kwa Ksh163 kutoka Ksh165 huku Mafuta ya Taa yakishushwa hadi Ksh146 kutoka Ksh147.94.

Bei hizo mpya zitaanza kutumika kuanzia Oktoba 14 saa sita usiku kwa muda wa mwezi mmoja.

Bei hizo ni pamoja na asilimia 8 ya ushuru wa Ongezeko la Thamani ya bidhaa (VAT).