Watu 2 wajeruhiwa baada ya kuhusika katika ajali ya ndege Baringo

Wawili hao walikimbiwa hopitalini ili kupokea matibabu.

Muhtasari
  • Ndege hiyo ilianguka Jumapili wakati ikijiandaa kutua katika uwanja wa ndege wa Kampi ya Samaki, ulio karibu na Ziwa Baringo

Wanaume wawili wamenusurika kifo baada ya ndege ndogo waliyokuwa wameabiri kuanguka katika Kaunti ya Baringo.

Ndege hiyo ilianguka Jumapili wakati ikijiandaa kutua katika uwanja wa ndege wa Kampi ya Samaki, ulio karibu na Ziwa Baringo.

Mhifadhi wa Ziwa Baringo Jackson Komen alithibitisha kuwa wawili hao walipata majeraha, kwani ndege hiyo ilikuwa imeharibika vibaya.

Chanzo cha ajali bado hakijajulikana.

Wawili hao walikimbiwa hopitalini ili kupokea matibabu.