Mahakama yazuia CAS kupata mshahara

Jaji Hedwig Ong'undi pia amewazuia kwa muda walioteuliwa kupata mshahara, malipo au manufaa yoyote.

Muhtasari
  • Shughuli hiyo ilianza mwendo wa saa 7:00 asubuhi, huku viongozi, wateule na wanafamilia wao wakiwa kwenye ukumbi huo.
Mahakama
Mahakama
Image: MAHAKAMA

Mahakama Kuu mnamo Ijumaa ilitoa agizo ya kuzuia mishahara ya Makatibu Wandamizi  (CAS) 50 walioapishwa siku ya Alhamisi.

Jaji wa Mahakama kuu Hedwig Ongudi alitoa uamuzi huo kufuatia ombi lililowasilishwa na Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK) na Shirika la Katiba Institute kupinga uhalali wa uteuzi huo.

Jaji Hedwig Ong'undi pia amewazuia kwa muda walioteuliwa kupata malipo yoyote na marupurupu mengine.

Rais William Ruto Alhamisi aliwaapisha Makatibu Waandamizi katika Ikulu ya Nairobi.

Shughuli hiyo ilianza mwendo wa saa moja asubuhi, huku viongozi, wateule na wanafamilia wao wakiwa kwenye ukumbi huo.

Miongoni mwa waliokula kiapo ni Evans Kidero, Millicent Omanga, Denis Itumbi, Nicholas Gumbo, na Isaac Mwaura.

Wengine walikuwa Cate Waruguru, Samuel Tanui na Charles Njagua.