Mkewe Chebukati ateuliwa kuwa mwenyekiti wa CRA

Wanyonyi aliteuliwa kutoka kundi la majina matatu yakiwemo ya Thomas Ludindi Mwadeghu na Felicity

Muhtasari
  • Katika taarifa, Rais alibainisha kuwa Wanyonyi alikuwa mgombeaji wa nafasi hiyo kwa sababu ya historia yake ya elimu na tajriba ya awali ya kitaaluma.
MARY WANYONYI
Image: KWA HISANI

Rais William Ruto mnamo Jumanne, Mei 23, alimteua Mary Wanyonyi  kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ugavi wa Mapato (CRA).

Katika taarifa, Rais alibainisha kuwa Wanyonyi alikuwa mgombeaji wa nafasi hiyo kwa sababu ya historia yake ya elimu na tajriba ya awali ya kitaaluma.

Wanyonyi aliteuliwa kutoka kundi la majina matatu yakiwemo ya Thomas Ludindi Mwadeghu na Felicity Nkirote Biriri ambayo yalikuwa yametumwa kwake na Tume ya Utumishi wa Umma (PSC)

“Mkuu wa Nchi kwa mujibu wa Kifungu cha 215 (2)(a) cha Katiba amemteua CPA Mary A.C. Wanyonyi kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ugavi wa Mapato (CRA).

"Bi. Wanyonyi ni Mhasibu Aliyeidhinishwa na Mpatanishi Aliyeidhinishwa ambaye pia ana Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara na Shahada ya Biashara (Uhasibu). Mteule huyo amekuwa na taaluma ya hali ya juu katika uhasibu unaochukua zaidi ya miongo mitatu," taarifa hiyo ilisoma kwa sehemu.