Mahakama ya rufaa yaondoa agizo la kusimamisha sheria ya fedha 2023

Katika uamuzi uliotolewa Ijumaa, Julai 28, Jaji Mohammed Warsame anasema rufaa iliyowasilishwa na Waziri wa Hazina ina umuhimu.

Muhtasari
  • Jaji Mkuu Martha Koome  alikuwa ameteua benchi la majaji 3 kusikiliza na kuamua malalamishi ya kupinga Sheria ya Fedha ya 2023.
Mahakama
Mahakama
Image: MAHAKAMA

Mahakama ya Rufaa imeondoa maagizo yanayozuia utekelezaji wa Sheria ya Fedha ya 2023 kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa rufaa hiyo.

Katika uamuzi uliotolewa Ijumaa, Julai 28, Jaji Mohammed Warsame anasema rufaa iliyowasilishwa na Waziri wa Hazina ina umuhimu.

“Msuko wa uamuzi wetu ni kwamba maombi hayo yana mashiko na yanaruhusiwa kama ilivyoombewa na kwamba agizo lililotolewa Julai 10, 2023 la kusimamisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2023, na amri inayokataza utekelezaji wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2023. na inaondolewa ikisubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa rufaa. Gharama zitaambatana na matokeo ya rufaa," ilisoma sehemu ya uamuzi huo.

Jaji Mkuu Martha Koome  alikuwa ameteua benchi la majaji 3 kusikiliza na kuamua malalamishi ya kupinga Sheria ya Fedha ya 2023.

Majaji hao watatu ni Lawrence Mugambi, David Majanja na Christine Meori.

Benchi ambayo inaongozwa na David Majanja inlitarajiwa kubainisha kesi iliyowasilishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah na wengine sita.