Mkurugenzi mkuu wa CA Ezra Chiloba asimamishwa kazi

Kutokana na hali hiyo, Christopher Wambua ameteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu.

Muhtasari
  • Notisi kutoka kwa mwenyekiti wa bodi Mary Mungai aliwasilisha kusimamishwa kwake siku ya Jumatatu katika taarifa kufuatia mkutano wa bodi.
Ezra Chiloba
Ezra Chiloba
Image: Twitter

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya Ezra Chiloba amesimamishwa kazi.

Notisi kutoka kwa mwenyekiti wa bodi Mary Mungai aliwasilisha kusimamishwa kwake siku ya Jumatatu katika taarifa kufuatia mkutano wa bodi.

Kutokana na hali hiyo, Christopher Wambua ameteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu.

“Kufuatia kikao cha Bodi ya Mamlaka kilichofanyika tarehe 18 Septemba 2023, na kusababisha Mkurugenzi Mkuu kusimamishwa kazi, ninayofuraha kuwajulisha wafanyakazi wote kuhusu uteuzi wa Bw.Christopher Wambua kama Mkurugenzi Mkuu katika Kaimu Nafasi yake kuanzia leo hadi nitakapotangazwa tena. imani kwamba utampa usaidizi unaohitajika," Mungai alisema katika taarifa yake