Wafahamu magavana waliotimuliwa na mabunge ya kaunti

Zaidi ya magavana 10 hata hivyo wamewahi kupigiwa kura ya kutimuliwa.

Muhtasari

•Wabunge 67 kati ya 69 wa Bunge la Kaunti ya Meru waliipigia kura ya kumtimua gavana wa kaunti hiyo Kawira Mwangaza.

•Ikiwa seneti itaidhinisha kutimuliwa kwa Kawira, basi atakuwa gavana wa nne kuondolewa mamlakani nchini Kenya

Image: HILLARY BETT

Jumatano jioni, Wabunge 67 kati ya 69 wa Bunge la Kaunti ya Meru waliipigia kura ya kumtimua gavana wa kaunti hiyo Kawira Mwangaza baada ya kinara wa walio wachache Mhe DMK Kiogora kuwasilisha hoja.

MCAs wa Meru waliwasilisha stakabadhi za kutimuliwa kwa Kawira Mwangaza kwa Seneti siku ya  Alhamisi na hatima ya gavana huyo wa muhula wa kwanza sasa iko mikononi mwa maseneta wa Kenya.

Ikiwa seneti itaidhinisha kutimuliwa kwa Kawira, basi atakuwa gavana wa nne kuondolewa mamlakani nchini Kenya. Zaidi ya magavana 10 hata hivyo wamewahi kupigiwa kura ya kutimuliwa na mabunge ya kaunti wanazoongoza, baadhi walinusuriwa na seneti huku wengine wakitumwa nyumbani.