Jinsi Man City inaweza Kuadhibiwa kwa Ukiukaji wa Kifedha

Man City huenda ikaadhibiwa vikali baada ya kupatikana na makosa zaidi ya 100 ya ukiukaji wa kifedha.

Muhtasari

•Mashtaka hayo yanahusiana na ukiukaji wa kanuni kwa misimu tisa kati ya 2009 na 2018, huku uchunguzi ukianza Desemba 2018.

Jinsi Man City inaweza kuadhibiwa kwa ukiukaji wa kifadha
Image: HILLARY BETT

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya EPL, Manchester City huenda wakafukuzwa kutoka kwenye ligi kuu ya EPL baada ya kupatikana na makosa zaidi ya 100 ya kukiuka masharti ya kifedha kwa muda mrefu.

Mashtaka hayo yanahusiana na ukiukaji wa kanuni kwa misimu tisa kati ya 2009 na 2018, huku uchunguzi ukianza Desemba 2018.

Uchunguzi wa klabu hiyo umedumu kwa miaka minne.