Wafahamu wanasoka waliokufa chini ya mazingira yasiyo ya kawaida

Kikosi kizima cha Timu ya Taifa ya Zambia kilipoteza maisha katika ajali ya ndege mwaka 1993.

Muhtasari

•Atsu ni miongoni mwa maelfu ya watu ambao wamepoteza uhai kufuatia tetemeko la ardhi ambalo lilikumba nchi ya Uturuki.

•Wachezaji 8 wa klabu ya Manchester United walifariki baada ya kuhusika katika ajali ya ndege mnamo Februari 6, 1958.

Hivi majuzi, habari za kuhuzunisha za kifo cha mchezaji wa Hatayspor, Christian Atsu, ambaye alipatikana amefariki chini ya vifusi vya nyumba katika mji wa Hatay zilivunja mioyo ya wengi kote duniani.

Atsu ni miongoni mwa maelfu ya watu ambao wamepoteza uhai kufuatia tetemeko la ardhi ambalo lilikumba nchi ya Uturuki mapema mwezi huu na kupelekea nyumba nyingi kuporomoka.

Kando na Atsu, kumekuwa na wachezaji wengine wengi ambao wamepoteza maisha yao ghafla  katika mazingira yasiyo ya kawaida.

Mnamo Aprili 27, 1993, ndege ya Jeshi la Wanahewa la Zambia iliyokuwa imebeba kikosi kizima cha timu ya taifa hilo (Chipolopolo) na wasaidizi wa kikosi  ilianguka katika Bahari ya Atlantiki muda mfupi baada ya kupaa kutoka Libreville, Gabon. Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu 30 wakiwemo wachezaji 18.

Wachezaji 8 wa klabu ya Manchester United walifariki baada ya kuhusika katika ajali ya ndege mnamo Februari 6, 1958.