Maeneo ambayo kupiga picha ni marufuku nchini Kenya

Huruhusiwi kupiga picha katika ofisi kuu za serikali kama vile Harambee House, Harambee Annex.

Muhtasari

•Miss Trudy, alizua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kudai alinyanyaswa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi, Mombasa kwa kurekodi video.

•Ni marufuku kupiga picha katika Makao Makuu ya Jeshi na ya polisi.

Image: WILLIAM WANYOIKE

Siku ya Jumatano, mtayarishaji wa maudhui wa Kenya, Gertrude Awino Juma, almaarufu Miss Trudy, alizua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kudai alinyanyaswa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi, Mombasa kwa kurekodi video.

Kile ambacho Bi Trudy huenda hakujua ama alipuuza, kupiga picha na video katika uwanja wa ndege ni marufuku nchini Kenya.