Wafahamu Wakenya mashuhuri waliosali katika ukuta wa Jerusalem

Rais mstafu Uhuru Kenyatta, Raila Odinga na mwanahabari Dennis Okari ni baadhi tu ya walioomba katika ukuta huo.

Muhtasari

•Katika picha zilizosambazwa siku za Jumatano, rais na mkewe walionekana wakiinama kwa maombi katika eneo hilo.

•Mwaka wa 2016, rais mstaafu Uhuru Kenyatta alifanya ziara ya kutembelea ukuta huo ambapo alifanya maombi.

mashuhuri waliosali katika ukuta wa Jerusalem
Wakenya mashuhuri waliosali katika ukuta wa Jerusalem
Image: WILLIAM WANYOIKE

Rais William Ruto na mkewe Rachel Ruto walitembelea Ukuta wa Wailing Wall mjini Jerusalem  wakati wa ziara yake nchini Israel.

Katika picha zilizosambazwa siku za Jumatano, rais na mkewe walionekana wakiinama kwa maombi katika eneo hilo.

Eneo hilo lililo katika jiji la kale la Jerusalemu ni ukuta wa mwisho uliobaki wa nje wa hekalu la kale la Kiyahudi na ni eneo muhimu sana la historia ya kisasa ya Israeli. Ni bure kwa kila mtu  na iko wazi masaa 24.

Rais na mkewe sio Wakenya wa kwanza  kuwahi kufanya maombi mbele ya ukuta huo.

Mwaka wa 2016, rais mstaafu Uhuru Kenyatta alifanya ziara ya kutembelea ukuta huo ambapo alifanya maombi.

Kiongozi wa Azimio-One Kenya, Raila Odinga alifika katika eneo hilo mwaka wa 2017 ambapo aliomba.