Wafahamu wachezaji wa EPL walioadhibiwa vikali kwa makosa ya kamari (betting)

Trippier, Townsend ni miongoni mwa wachezaji wengine ambao waliwahi kupatikana na makosa kama hayo na kuadhibiwa.

Muhtasari

•Ivan Toney wa Brentford alipigwa marufuku ya miezi 8 na kupigwa faini ya Ksh8.5m baada ya kupatikana na makosa  232 yanayohusiana na kamari.

Wachezaji wa EPL walioadhibiwa kwa makosa ya kamari (betting)
Image: ROSA MUMANYI

Hivi majuzi, mchezaji wa Brentford Ivan Toney alipigwa marufuku ya miezi minane na kupigwa faini ya milioni 8.5 baada ya kupatikana na makosa  232 yanayohusiana na kamari.

Ivan Toney sio mchezaji wa kwanza kuadhibiwa kwa makosa ya kamari; Sturridge, Trippier, Townsend ni miongoni mwa wachezaji wengine wa Ligi Kuu ambao waliwahi kupatikana na makosa kama hayo na kuadhibiwa vikali.