Wasanii wanaume waliowahi kuvalia mavazi ya kike ili kutumbuiza mashabiki wao

Mwimbaji wa Injili, Chris Embarambamba hivi majuzi alionekana akiwa amevalia rinda, sidiria na wigi kichwani.

Muhtasari

•Embarambamba, Dulla Makabila na Bahati ndio wasanii walioonekana hivi majuzi wakiwa wamevalia mavazi ya kike hadharani.

Wasanii wanaume waliowahi kuvalia mavazi ya kike
Image: HILLARY BETT

Hivi majuzi kumekuwa na mtindo wa wasanii wa kiume kuvaa mavazi ya kike kwa nia ya kuwaburudisha mashabiki wao.

Embarambamba, Dulla Makabila na Bahati ndio wasanii walioonekana hivi majuzi wakiwa wamevalia mavazi ya kike hadharani.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Chris Embarambamba hivi majuzi alionekana akiwa amevalia rinda, sidiria na wigi kichwani.

Staa wa Bongo, Dulla Makabila alionekana jukwaani akiwa amevalia wigi na kujipondoa usoni.