Fahamu kaunti ambazo wanawake walipoteza ubikira na umri mdogo zaidi

Utafiti huo ulifanywa kwa wanaume wenye umri wa miaka 25 hadi 54.

Muhtasari

•Samburu inaongoza kwa umri wa chini kabisa ambapo wanawake walishiriki mapenzi kwa mara ya kwanza

Kaunti ambazo wanawake walipoteza ubikira na umri wa chini kabisa
Image: WILLIAM WANYOIKE

Kaunti ya Samburu inaongoza kwa umri wa wastani wa chini kabisa ambapo wanawake walishiriki mapenzi kwa mara ya kwanza nchini Kenya.

Utafiti wa Demografia na Afya ya Kenya 2022 (KDHS 2022) uliofanywa na KNBS unaonyesha kuwa wanawake katika kaunti hiyo ya mkoa wa bonde la ufa walishiriki tendo la ndoa kwa mara ya kwanza wakiwa na umri wa wastani wa miaka 15.6.

Kaunti ya West Pokot inafuatia kwa umri wa wastani wa chini kabisa ambapo wanawake walifanya ngono kwa mara ya kwanza, miaka 15.7.

Utafiti huo ulifanywa kwa wanaume wenye umri wa miaka 25 hadi 54.