Wafahamu wachezaji soka waliostaafu baada ya miaka 40

Wastani wa umri wa kustaafu wa wachezaji wa soka duniani ni takriban miaka 35.

Muhtasari

•Gianluigi Buffon alitangaza kustaafu soka siku ya Jumatano, Agosti 3 baada ya kucheza kwa miaka 28.  

•Buffon sio mwanasoka wa kwanza kustaafu baada ya miaka 40, wengine waliostaafu baada ya miaka 40 wameorodheshwa kwenye grafiki ya leo

Wachezaji soka bora waliostaafu baada ya miaka 40.
Image: HILLARY BETT

Kipa wa Italia Gianluigi Buffon alitangaza kustaafu soka siku ya Jumatano, Agosti 3 baada ya kucheza kwa miaka 28.  

Buffon ni miongoni mwa wachezaji wa soka waliostaafu na umri mkubwa zaidi baada ya kutundika glavu zake akiwa na umri wa miaka 45. Wastani wa umri wa kustaafu wa wachezaji wa soka duniani ni takriban miaka 35, kumaanisha kwamba amecheza kwa bonasi ya takriban miaka 10 zaidi.

Hata hivyo, Buffon sio mchezaji wa soka wa kwanza kustaafu baada ya miaka 40, wengine bora waliostaafu baada ya miaka 40 wameorodheshwa kwenye grafiki ya leo.