Fahamu mfanano mkubwa kati ya Kajala na mpenzi mpya wa Harmonize, Phiona

Phiona ana sifa kadhaa ambazo zinafanana na za aliyekuwa mpenzi wa Harmonize, Frida Kajala Masanja.

Muhtasari

•Harmonize alifichua kuwa amemnunulia mrembo huyo mwenye umbo wa kuvutia gari nyeupe aina ya Velar Range Rover.

•Mwanamitindo huyo mrembo na mshawishi wa Instagram anajulikana kwa misemo yake ya kuvutia 'Wake Pray Slay' na 'Sweeter than honey."

kati ya Kajala na mpenzi mpya wa Harmonize, Phiona.
Mfanano kati ya Kajala na mpenzi mpya wa Harmonize, Phiona.
Image: WILLIAM WANYOIKE

Jumanne, staa wa Bongo, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize alithibitisha mapenzi yake mazito kwa mwanasosholaiti wa Rwanda Phiona almaarufu Yolo The Queen kwa njia ya kipekee na ya gharama kubwa.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alifichua amemnunulia mrembo huyo mwenye umbo wa kuvutia gari nyeupe aina ya Velar Range Rover.

Phiona anasemekana kuwa mmoja wa wanasosholaiti waliofanikiwa zaidi nchini Rwanda na vitongoji  vyake. Ameweza kunasa umakini wa watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii haswa wanaume, kwa hisani ya mwili wake wa kipekee uliopinda.

Mwanamitindo huyo mrembo na mshawishi wa Instagram anajulikana kwa misemo yake ya kuvutia 'Wake Pray Slay' na 'Sweeter than honey."

Mrwanda huyo ana sifa kadhaa ambazo zinafanana na aliyekuwa mpenzi wa Harmonize, Frida Kajala Masanja. 

Katika grafiki ya leo, tumeangazia mfanano mkubwa kati ya Phiona na Kajala.