Sababu za mahakama kuharamisha ushuru wa nyumba

Mahakama iliamuru wakenya kuendelea kutozwa ushuru wa nyumba hadi januari 10,2024

Muhtasari

• Jopo la majaji watatu liliafikia uamuzi kuwa sheria iliyotumika kutoza wakenya ushuru wa nyumba haikufuata taratibu za kisheria

• Mswada wa Fedha wa 2023 ulipitishwa na bunge mnamo Juni 22, 2023, na baadaye kuidhinishwa na Rais William Ruto mnamo Juni 26.

Image: ROSA MUMANYI

Jopo la majaji watatu lililojumuisha Majaji David Majanja, Lawrence Mugambi na Christine Meoli pia lilitangaza vifungu vya 84, 72 hadi 78 vya Sheria ya Fedha kuwa batili.