Kelvin Kiptum: Mfahamu mwanariadha ambaye amefariki miezi baada ya kuvunja rekodi ya dunia

Kiptum alipoteza maisha yake katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea kwenye barabara ya Eldoret-Kaptagat Jumapili usiku.

Muhtasari

•Kiptum alivunja rekodi ya dunia ya marathon mwezi Oktoba, mwaka jana alipokimbia kwa saa 2:00:35 katika Chicago Marathon.

•Marehemu ni mwanariadha wa kwanza kukimbia marathon chini ya saa mbili na dakika moja, alivunja rekodi ya Eliud Kipchoge kwa sekunde 34 .

 

alifariki siku ya Jumapili, Februari 11, 2024.
Kelvin Kiptum alifariki siku ya Jumapili, Februari 11, 2024.
Image: WILLIAM WANYOIKE

Kiptum ,24, na kocha wake raia wa Rwanda Gervais Hakizimana walifariki papo hapo kufuatia ajali mbaya iliyotokea umbali mfupi sana kutoka kijiji chake cha Chepsamo, magharibi mwa Kenya.

Kiptum alivunja rekodi ya dunia ya marathon mwezi Oktoba, mwaka jana alipokimbia kwa masaa 2:00:35 katika Chicago Marathon, na kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia marathon chini ya saa mbili na dakika moja, na kuchukua sekunde 34 chini ya rekodi ya awali ya Mkenya mwenzake Eliud Kipchoge.