Kutana na Mkenya mbunifu anayezalisha petroli kwa kutumia taka za plastiki

James na wenzake hukusanya taka za plastiki, kuzichambua kabla hawajaanza mchakato wa kuzichemsha ili kuongeza mafuta.

Muhtasari

 
Plastiki zilizosagwa huwekwa kwenye tanuri kwa ajili ya kuchakata.

Mchakato huo huchukua kati ya saa 24 hadi 36, kutegemeana na uzito wa plastiki hizo.

Image: BBC

Mkenya James Muritu amezitengenezea jina la kiheshima kwa juhudi zake za kufumbua mbinu ya kubadilisha takataka za plastiki na kuwa mafuta ya petroli na dizeli.

Katika mahojiano na TRT Afrika, Muritu alieleza jinsi ameweza kubuni teknolojia hiyo ambayo inatajwa kuwa ni mchakato rafiki kwa mazingira.

"Nilikuwa nikitengeneza vitalu vya kabro kutokana na taka za plastiki, na wakati wa majaribio yangu niliona namna plastiki zinavyoshika moto lilinishangaza," anaiambia TRT Afrika.

Ugunduzi huo ulimfanya Muritu aachane na utengenezaji wa vitalu hivyo na kuamua kuanza kuzalisha mafuta kupitia plastiki zilizoyeyushwa.

Alifanikiwa kufanya hivyo kwa kuziyeyusha plastiki kupitia nyuzi joto za juu kabisa.

"Baada ya kupata mafuta hayo, nilijaribu kuyatumia katika vyombo tofauti kama vile majenereta," Muritu alieleza kama alivyonukuliwa na TRT Afrika.

Kwa sasa, Muritu ni mwanzilishi wa kampuni ya Progreen Innovations, iliyojikita katika kuzalisha mafuta kupitia taka za plastiki.

"Nilijaribu kutumia mafuta hayo kwenye mashine ya kukatia majani na ilifanya kazi kwa ufanisi mkubwa."

Ubunifu huu unalenga kutatua tatizo la taka za plastiki duniani.

James na wenzake hukusanya taka za plastiki, kuzichambua kabla hawajaanza mchakato wa kuzichemsha ili kuongeza mafuta.

Plastiki zilizosagwa huwekwa kwenye tanuri kwa ajili ya kuchakata.

Mchakato huo huchukua kati ya saa 24 hadi 36, kutegemeana na uzito wa plastiki hizo.

"Tunachofanya ni kinyume na uchomaji moto," James anaelezea TRT Afrika.

"Pamoja na uchomaji, kuna moshi mwingi, na harufu ya sumu ya plastiki inayoungua inajaza hewa. Hakuna gesi inayotolewa katika mchakato wetu, na tunaendelea kutafiti hilo ili kuhakikisha kuwa haina kaboni kwa asilimia 100.