Kareh B: Mfahamu kwa undani mwanamuziki ambaye mwanawe alifariki ajali ya Easy Coach

Mwanawe Kareh B, Joseph Maduli alifariki katika ajali ya Easy Coach iliyotokea Kisumu mnamo Aprili 1, 2024

Muhtasari

•Mtoto wa Kareh B mwenye umri wa miaka 17, Joseph Maduli alifariki baada ya basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa shule ya upili ya Chavakali kuanguka katika eneo la Mamboleo, Kisumu.

Mfahamu Kareh B
Image: ROSA MUMANYI

Mwanawe Kareh B, Joseph Maduli alifariki katika ajali iliyotokea Aprili 1, 2024

• Jina halisi ni Mary Wangari Gioche.

• Alizaliwa na kukulia Kaunti ya Murang'a.

• Mzaliwa wa mwisho katika familia ya ndugu wanne.

• Anajulikana zaidi kwa kolabo zake na Jose Gatutura.

• Alipata umaarufu 2018 kutokana na wimbo ‘Tuirio twega’.

• Alimpoteza dadake, aliyekuwa mwanahabari wa NTV Winnie Mukami, 2021.

• Nyimbo zake maarufu; 'Tuirio Twega, Haha ni Gute, na 'Mwari Wa Muthamaki'

Chanzo: Mahojiano ya awali na Word Is