Homeboyz radio yawafuta kazi Shaffie, Joe Mfalme na Neville

shaffie, dj joe mfalme na neville
shaffie, dj joe mfalme na neville

Redio ya Homeboyz ambayo iko chini ya usimamizi wa kampuni ya Redio Afrika, imewasimamisha kazi Shaffie Weru, Joseph Munoru (DJ Mfalme) na Neville Muysa.

Kufutwa kazi kwao kunafuatia ukaguzi kamili wa maoni yaliyotolewa kwenye kituo hicho Alhamisi asubuhi na baadaye wakasimamishwa kazi.

"Washirika wetu na wasikilizaji hawatashangazwa na hatua hii ya kuwasimamisha kazi kwani ni jambo sahihi la kufanya," Meneja Mkuu wa Redio ya Homeboyz Somoina Kimonjino alisema katika taarifa Jumamosi jioni.

 

Aliongeza; "Maoni ya wafanyikazi hao wa zamani wakati huo hayakuidhinishwa na kampuni hiyo wala mada haikujadiliwa au kuidhinishwa na uongozi wa kampuni hiyo. Tumevunjika moyo sana kwa tabia hizo."

Siku ya Ijumaa, watatu hao walisimamishwa kazi kwa muda wa wiki mbili kuhusiana na maoni waliyotoa ambayo yalionekana kumuaibisha mwathiriwa na kuhalalisha unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake.

Kimonjino alisema kuwa uchunguzi umeamua kwamba mwenendo wao ni utovu wa nidhamu na ukiukaji mbaya wa sera za kampuni hiyo.

"Kampuni  hiyo haiungi mkono unyanyasaji wa kijinsia au aina yoyote ya unyanyasaji wa mwili, matusi na kihemko wala haiungi mkono maoni yaliyotolewa na wafanyikazi hao watatu," alisema.

Aliishukuru Kenya kwa kudai zaidi tasnia ya habari kwa jumla.