'Jaribio la mapinduzi' Guinea-Bissau lalaaniwa

Muhtasari
  • Umoja wa Mataifa na viongozi wa kikanda wamelaani makabiliano yaliyosababisha mauaji katika mji mkuu

Jumuiya ya kiuchumi na kisiasa katika nchi za Afrika Magharibi Ecowas, imelaani kile inachokiita "jaribio la mapinduzi" nchini Guinea-Bissau, na imeilitaka jeshi kurejea katika kambi zake.

Hii inafutia ripoti za watu waliokuwa wamevalia nguo za kiraia kufyatua risasi karibu na jengo la serikali ambamo rais alikuwa akifanya mkutano na waziri mkuu Guinea-Bissau, wambaye bado haijafahamika yuko wapi.

Wakati haya yakijiri , mwandishi wa habari nchini Guinea Bissau ameiambia BBC kuwa wanajeshi waliojitenga wamemshikilia rais wa Guinea-Bissau na mawaziri wake.

Haijawezekana kuthibisha madai haya kwa vyanzo huru, na hakuna taarifa rasmi ambayo imetolewa bado juu y ani wapi alipo rais wa Guinea na waziri mkuu.

Lakini mwandishi wa habari Alberto Dabo amekiambia kipindi cha redio cha BBC- BBC Focus on Africa kwamba"vyanzo vya kuaminika vinasema kwamba Umaro Sissoco Embaló na wajumbe wengine wa serikali yake bado wako katika kasri la serikali na wako mikononi mwa washambuliaji ".

Umoja wa Mataifa na viongozi wa kikanda wamelaani makabiliano yaliyosababisha mauaji katika mji mkuu na kutaka taasisi za kidemokrasia ziheshimiwa. Polisi mmoja ameuawa.

Kumekuwa na mapinduzi kadhaa katika mataifa ya Afrika Magharibi katika kipindi cha miezi 18, huku jeshi likinyakua madaraka katika mataifa ya Mali, Guinea na Burkina Faso.