Tanzia:Oprah Winfrey aomboleza kifo cha baba yake

Oprah alitangaza kifo cha babake katika taarifa kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii siku ya Jumamosi.

Muhtasari
  • Oprah alitangaza kifo cha babake katika taarifa kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii siku ya Jumamosi
  • Vernon Winfrey alifariki siku ya Ijumaa baada ya kuugua saratani akiwa na umri wa miaka 89

Babake Oprah Winfrey, Vernon Winfrey, amefariki.

Vernon Winfrey alifariki siku ya Ijumaa baada ya kuugua saratani akiwa na umri wa miaka 89.

Oprah alitangaza kifo cha babake katika taarifa kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii siku ya Jumamosi.

Nyota huyo wa televisheni mwenye umri wa miaka 68 alichapisha video ya heshima kwa babake Vernon Winfrey kwenye Instagram wakisimulia matukio yao ya mwisho.

"Vernon Winfrey 1933-2022.

Chini ya wiki moja iliyopita tulimheshimu baba yangu katika uwanja wake wa nyuma. Rafiki yangu na mwimbaji wa nyimbo za injili Wintley Phipps alimsalimia kwa wimbo.

ALIHISI mapenzi na kuyafurahia hadi akashindwa kuongea tena.

Jana pamoja na familia iliyozunguka kando ya kitanda chake, nilipata heshima takatifu ya kushuhudia mtu aliyehusika na maisha yangu, akivuta pumzi yake ya mwisho.

Tuliweza kuhisi Amani ikiingia chumbani kwa kupita kwake. Amani hiyo bado ipo. Yote ni sawa. Asante kwa maombi yako na mawazo mazuri."

Kutoka kwetu wanajambo Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.