(+video) Mhandisi atengenezea nyoka wake robot ya miguu kumwezesha kutembea na si kutambaa

Allen Pan aliipakia video hiyo kwenye YouTube yake ikiwa namada ‘Kuwarudishia miguu yao nyoka’

Muhtasari

• Allen Pan ambaye pia kando kuwa mhandisi na mpenzi wa nyoka ni MwanaYouTube ambaye alitengeneza miguu minne ya roboti kwa nyoka ili aweze kutembea.

Mwanayoutuber huyo aliunda miguu kwa ajili ya nyoka wake
Mwanayoutuber huyo aliunda miguu kwa ajili ya nyoka wake
Image: YouTube screengrab

Duaniani kila sekunde iendayo kwa Mungu, ina miujiza yake ambayo inafanyika. Je, wewe msomaji wetu tukuulize tu swali la kzushi, umewahi kuona nyoka akitembea? Hapana, sawa?

Sawa, amini usiamini, kuna video inasambaa ikionyesha nyoka 'akitembea'. Hapana, hatutanii! Lakini sivyo unavyofikiri.

Nchini Marekani kuna mwanaume mmoja mhandisi ambaye pia anajiongeza kama mpenzi wa ufugaji nyoka amemtengenezea nyoka wake robot ya miguu ili kumfanya aache kutambaa na badala yake kutembea kwa miguu hiyo ya robot.

Allen Pan ambaye pia kando kuwa mhandisi na mpenzi wa nyoka ni MwanaYouTube ambaye alitengeneza miguu minne ya roboti kwa nyoka ili aweze kutembea.

Video yake inaonyesha jinsi alivyopanga kutengua mamilioni ya miaka ya mageuzi ili kuwapa nyoka miguu yao na aliipakia kwenye YouTube yake ikiwa namada ‘Kuwarudishia miguu yao nyoka’

Pan alisema lengo la mradi huo ni kuthibitisha kuwa yeye ni "mpenzi wa nyoka" baada ya kuitwa mnyanyasaji kwa kukamata na kumwachia nyoka mwitu.

"Wakati mnyama mwingine yeyote ana ulemavu wa miguu, ubinadamu hukusanyika ili kumlaani Mungu usoni na tunamtengenezea mnyama huyo miguu mipya ya kupendeza. Lakini hakuna mtu anapenda nyoka vya kutosha kuwajengea miguu ya roboti. Hakuna mtu isipokuwa mimi" Pan alisema kwenye video yake ya YouTube.

Pan aliunda miguu minne ya nyoka bandia ambayo inaweza kutembea. Katika video hiyo, alielezea jinsi alivyoenda kugeuza mamilioni ya miaka ya mageuzi ili kutoa miguu ya nyoka.

Wakati wa kutengeneza video hiyo, Pan aligundua kuwa nyoka huwa na miguu wakiwa katika hatua ya kiinitete kisha kuipoteza katika hatua ya baadaye ya ukuaji.

Alionyesha jinsi alivyojipanga kutengeneza kifaa ambacho nyoka wanaweza kutumia ili “kutembea,” huku sharti moja likiwa ni lazima nyoka huyo aweze kuingia kwa uhuru na kutoka ndani ya kifaa hicho akiwa peke yake.

Kuelekea mwisho wa video, Pan anamtembelea mfugaji wa nyoka ambaye anakubali kuazima chatu ili kujaribu mashine hiyo.

Chatu anaishia kuteleza kwenye bomba, ambalo hudhibitiwa na Pan. Nyoka mwenyewe hakuwa na udhibiti juu ya miguu.Wakati wa majaribio, nyoka alikaa kwa hiari ndani ya mashine, inaonekana aliridhika na kutembezwa kwa miguu.

"Na sasa unaweza kumtembeza nyoka wako, kama vile Mungu hakutaka kamwe," Pan anasema kwenye video.