Museveni alaani nchi za Magharibi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi

Uganda inatazamiwa kuanza kuuza mafuta nje ndani ya miaka mitatu.

Muhtasari

•Bw Museveni aliangazia kuvunjwa kwa sehemu ya shamba la upepo nchini Ujerumani ili kutoa nafasi ya upanuzi wa mgodi wa makaa ya mawe.

Image: BBC

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amezishutumu nchi za Magharibi kwa kutowajibika linapokuja suala la ahadi za kukomesha mabadiliko ya hali ya tabianchi.

Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii, Bw Museveni aliangazia kuvunjwa kwa sehemu ya shamba la upepo nchini Ujerumani ili kutoa nafasi ya upanuzi wa mgodi wa makaa ya mawe.

Alisema hatua hiyo ilifanya dhihaka kwa ahadi za Magharibi kuelekea malengo ya hali ya hewa. Kiongozi huyo wa Uganda pia alisema nchi za Ulaya zinafurahia kuchukua rasilimali za Afrika kwa mahitaji yao ya nishati lakini zinapinga maendeleo ya miradi ya mafuta ambayo ilikuwa kwa manufaa ya Waafrika.

Uganda inatazamiwa kuanza kuuza mafuta nje ndani ya miaka mitatu.

Kutokana na msukosuko wa nishati duniani baadhi ya nchi za Ulaya hivi karibuni zimeamua kuongeza uzalishaji wa makaa ya mawe hatua ambayo ilishutumiwa vikali na wanaharakati wa mabadiliko ya tabianchi.