Zelensky asema ajali ya helikopta iliyowaua maafisa wa ngazi ya juu ‘ilitokana na vita’

Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine Denys Monastyrsky alifariki, pamoja na wenzake wengine kadhaa.

Muhtasari

Ajali ya helikopta  ya Jumatano ilitokea karibu na shule ya chekechea katika eneo la   Brovary.

Image: GIAN EHRENZELLER/EPA

Rais wa Ukraine  Volodymyr Zelensky  amesema kuwa  " hakuna ajali wakati wa vita"baada ya watu 14 kufariki katika ajali ya helikopta iliyoanguka katika mji mkuu, Kyiv.

Ukraine haijadai uhusika wa Urusi, lakini Bw Zelensky aliuambia Mkutano wa Dunia wa Uchumi mjini Davos kwamba ajali hiyo ilikuwa ni athari ya vita.

Waziri wa mambo ya ndani  wa Ukraine Denys Monastyrsky  alifariki, pamoja na wenzake wengine kadhaa.

Bw Zelensky pia alitumia hotuba yake ya video kuwataka washirika kutuma haraka silaha zaidi kabla ya mashambulizi mapya ya Urusi.

 "Muda ambao dunia huru inautumia kufikiria unatumiwa na taifa la kigaidi kuuua ," alieleza.Kauli hiyo ilitafsiriwa kwa ombo la Ujerumani ili kuharakisha usambazaji wa haraka wa vifaru vya kijeshi vya Leopard.

Berlin  imeripotiwa kutokuwa na utashi wa kutuma magari hayo mpaka Marekani ikubali kutoa vifaru vyake  vya kivita vinavyofahamika kama Abrams. Hivi karibuni Uingereza ilipeleka vifaru vyake kadhaa mjini Kyiv.     

 Mkuu wa muungano Wa Nato alisema katika mkutano wa Davos  Jumatano kwamba Ukraine inaweza kutarajia kupokea ‘’usaidizi zaidi’’, usaidizi wa kisasa zaidi, silaha nzito na silaha za kisasa zaidi ".

Bw Jens Stoltenberg  alisema kuwa nchi wanachama wa muungano wa Nato zitakutana Ijumaa kujadili ni vifaa gani vya kijeshi vinaweza kupelekwa Kyiv.

Ajali ya helikopta  ya Jumatano ilitokea karibu na shule ya chekechea katika eneo la   Brovary, nje ya mji wa Kyiv, majira ya saa mbili  kwa saa za Kyiv. Mmoja wa watu waliokufariki alikuwa ni mtoto.

 Bw  Monastyrsky, mwenye umri wa miaka 42, alikuwa ni mshauri wa muda mrefu zaidi wa kisiasa wa  Rais  Zelensky. Ni mtu mwenye cheo cha juu wa Ukraine  aliyefariki tangu vita vya Ukraine vianze. 

Kifo chake ni pigo kubwa kwa utendaji wa serikali ya Ukraine mjini  Kyiv kwani wizara ya mambo ya ndani ina jukumu muhimu la kuimarisha usalama na kuongoza shughuli  za polisi  wakati wa vita.   

 Sura yake ilitambuliwa miongoni mwa Waukraine katika kipindi chote cha vita , akitoa taarifa za mara kwa mara kwa umma kuhusu majeruhi  na vifo katika mji wa   Alon waliosababishwa na mashambulio ya makombora ya Urusi tangu ulipoanza uvamizi mwezi Februari 2022.   

Naibu mkuu wa ofisi yar ais nchini Ukraine Bw  Monastyrsky  amekuwa akisafiri katika maeneo "vitovu vya vita". Mkuu wa polisi katika Kharkiv aliongeza kuwa kikosi cha wizara ya mambo ya ndani kimekuwa  njiani kikieleka kukutana naye.

 Hakuna dalili kwamba ajali ilikuwa kitu kingine isipokuwa ajali 

 Lakini huduma za usalama za taifa  SBU zilisema kuwa zinaangalia uwezekano wa sababu kadhaa  - ikiwa ni pamoja na  hujuma, kasoro za kiufundi na ukiukaji wa sheria za safari za anga. 

Eneo la tukio baada ya helikopta ya Brovary kuanguka
Eneo la tukio baada ya helikopta ya Brovary kuanguka

Naibu mkuu wa ofisi yar ais nchini Ukraine Bw  Monastyrsky  amekuwa akisafiri katika maeneo "vitovu vya vita". Mkuu wa polisi katika Kharkiv aliongeza kuwa kikosi cha wizara ya mambo ya ndani kimekuwa  njiani kikieleka kukutana naye.

 Hakuna dalili kwamba ajali ilikuwa kitu kingine isipokuwa ajali 

 Lakini huduma za usalama za taifa  SBU zilisema kuwa zinaangalia uwezekano wa sababu kadhaa  - ikiwa ni pamoja na  hujuma, kasoro za kiufundi na ukiukani wa sheria za safari za anga. 

Maafisa muhimu mara kwa mara  husafirishwa kwa ndege  katika maeneo mbali mbali ya Ukraine kwa kimo cha mti ili kuepuka kubainika, lakini hilo pia lina hatari zake.   

Kile kilichotambuliwa cha helikopta hiyo ulikuwa ni mlango na moja ya mbawa zake ambavyo vilitua juu ya gari. Kando yake kulikuwa na miili mitatu iliyokuwa imefunikwa kwa blanketi  za dharura za ndege.    

Maafisa wengine waliofariki katika ajali ni pamoja na naibu wa kwanza wa waziri Yevhen Yenin na waziri wa nchi Yuriy Lubkovych, pamoja na Tetiana Shutiak,  msaidizi wa Bw Monastyrsky.

 Kufuatia ajali hiyo, Ihor Klymenko – mkuu wa kikosi cha taifa cha  Ukraine - aliteuliwa kuwa kaimu waziri wa mambo ya ndani.

Rafiki wa hayati waziri, Mbunge Mariia Mezentseva, alisema kuwa ni mkasa kwa kila mtu kwani wizara ilikuwa na nafasi muhimu kukabiliana na uvamizi nchini Ukraine.

"Alikuwa tayari kutoa usaidizi was aa 24 kwa siku saba za wiki kwa wafanyakazi wenzake, marafiki na familia. Alikuwa mtu wa karibu sana na Rais Zelensky kuanzia siku ya kwanza ya kampeni zake za urais," aliiambia BBC.

Rais wa marekani Joe Biden aliitaja ajali hiyo kama  "msiba wa kuvunja moyo".

Mashuhuda wengine walisema kuwa rubani alijaribu kuepuka majengo marefu kabal ya ajali, na badala yake akaenda karibu na shule ya chekechea. 

 "Wazazi walikuwa wanakimbia, wakipiga mayowe. Kulikuwa na mkanganyiko ," alisema mhudumu mkaazi ambaye alijitolea kutoa usaidizi  Lidiya. Huyduma za dharura na wakazi walikimbilia kuwaondosha watoto huku moto ukisambaa kwenye jengo la shule ya chekechea.  

Mkaazi mmoja, Dmytro,  alielezea kuruka juu ya uzio ili kuwasaidia watoto kutoka nje ya jengo. Alimchukua msichana mmoja ambaye baba yake hakumtambua kwani uso wake ulikuwa umejaa damu. 

Tukio hili linakuja siku nne baada ya Ukraine kupigwa na mashambulio mengine dhidi ya raia yaliyosababisha vifo tangu vita vianze.

Kombora la Urusi lilipiga jengo la gorofa katyika mji wa kati wa  Dnipro,na kuwauwa watu 45, wakiwemo watoto sita.   

Mabaki ya helikopta yaliongekana nje ya jengo la makazi katika
Mabaki ya helikopta yaliongekana nje ya jengo la makazi katika
Image: GETTY / UKRAINE MFA

Image: Picha ya setilaiti ya eneo la tukio la ajali