Mwalimu azuiliwa kwa tuhuma za mahusiano ya jinsia moja

Inayedaiwa kuwa mshirika wake ni mwenye umri wa miaka 30 ambaye si mwanafunzi wa shule hiyo wala hakuwa akiishi hapo.

Muhtasari
  • Msemaji wa Polisi wa Mkoa wa Kiira James Mubi alisema kwamba mwalimu huyo anachunguzwa kuhusiana na madai ya unyanyasaji wa kijinsia
Watu 24 wakamatwa katika msako dhidi ya LGBTQ Burundi.
Watu 24 wakamatwa katika msako dhidi ya LGBTQ Burundi.
Image: BBC NEWS

Mwalimu wa Uganda mwenye umri wa miaka 43 pamoja na anayedaiwa kuwa mpenzi wake bado wanazuiliwa baada ya kufika katika kituo cha polisi mwishoni mwa juma katika mji wa Jinja mashariki mwa nchi.

Mahusiano ya watu wa jinsia moja ni kinyume cha sheria nchini Uganda chini ya sheria za enzi za ukoloni, ambazo zimeimarishwa na miswada ya hivi majuzi zaidi ya kupinga mapenzi ya jinsia moja - ambayo ni ya hivi punde zaidi ambayo inaandaliwa na bunge.

Siku ya Ijumaa, wazazi wa wanafunzi katika shule ya Wasichana ya PMM walivamia jengo hilo wakitaka kuwaondoa watoto wao, huku kukiwa na madai ya mtandaoni wakimtuhumu mwalimu wa shule hiyo kwa kuendeleza uhusiano wa jinsia moja.

Msemaji wa Polisi wa Mkoa wa Kiira James Mubi alisema kwamba mwalimu huyo anachunguzwa kuhusiana na madai ya unyanyasaji wa kijinsia.

Inayedaiwa kuwa mshirika wake ni mwenye umri wa miaka 30 ambaye si mwanafunzi wa shule hiyo wala hakuwa akiishi hapo.

Pia alisema kufikia sasa hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa wanafunzi hao dhidi ya mwalimu huyo lakini ilikuwa ni lazima kuendelea kumshikilia yeye pamoja na anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake kwa usalama wao.

Zaidi ya wiki moja iliyopita, Waislamu wa Jinja na maeneo mengine ya nchi walitii wito wa Baraza Kuu la Waislamu wa Uganda kupinga kile wanachosema ni kuongezeka kwa uhusiano wa jinsia moja nchini humo.

Mwanaharakati wa haki za LGBTQ Frank Mugisha alionya wakati huo kwamba Uganda inaweza kushuhudia ongezeko la unyanyasaji dhidi ya watu walio katika mahusiano ya jinsia moja katika jamii.