Video ya kifo cha mwanaume mwenye asili ya Kenya inaonyesha polisi wakimfanyia ukatili – familia

Bw Otieno alifariki tarehe 6 Machi wakati alipokuwa akihamishwa kutoka gereza kupelekwa katika kituo cha afya

Muhtasari
  • Ripoti ya awali inaonyesha kuwa uchunguzi wa kimatibabu ulionyesha kuwa alifariki kwa - kukosa hewa, walisema waendeshamashitaka.

Mama wa mwanaume mweusi mwenye umri wa miaka 28 ambaye alifariki akiwa katika mahabusu ya polisi anasema video ya dakika 12 inayoonyesha tukio la mauaji yake inayo " sumbua na kutia kiwewe" na kisa hicho ni "ukatili".

Polisi saba wa cheo cha sheriff wa Virginia wameshitakiwa kwa mauaji ya daraja cha pili kuhusiana na kifo cha mwanaume huyo anayefahamika kama Irvo Otieno.

Waendesha mashitaka Alhamisi pia walitangaza mashitaka zaidi ya mauaji ya daraja la pili dhidi ya wafanyakazi watatu wa hospitali.

Wakili Crump alisema, katika video Otieno alionekana "akizuiliwa kwa ukatili mkubwa, huku akishindiliwa chini kwa goti kwenye shingo lake , akiwekewa uzito wa watu saba mwilini mwake, huku uso wake ukiangalia chini, akiwa amefungwa pingu."

Bw Crump amefananisha kisa cha Bw Otieno na tukio la George Floyd, Mmarekani mwingine mweusi aliyeuliwa kikatili na polisi.

Bw Otieno alifariki tarehe 6 Machi wakati alipokuwa akihamishwa kutoka gereza kupelekwa katika kituo cha afya cha watu wenye matatizo ya akili.

Ripoti ya awali inaonyesha kuwa uchunguzi wa kimatibabu ulionyesha kuwa alifariki kwa - kukosa hewa, walisema waendeshamashitaka.

Polisi saba wa Kaunti ya Henrico wameshutumiwa na waendeshamashitaka kwa kumuua Bw Otieno kwa kumkosesha hewa ya kupumua, wakati walipokuwa wakimhamisha.

Waendeshamashitaka wanasema ushahidi zaidi uliwawezesha pia kuwashitaki wafanyakazi wa hospitali katika Hospitali ya -Central State Hospital, ambako Bw Otieno alikuwa akihamishiwa.

Video ya tukio ilinaswa na kamera za usalama, na ilitazamwa Alhamisi na wakili maarufu wa haki za binadamu Ben Crump pamoja na familia ya Bw Otieno.

Mama yake Otieno, Caroline Ouko, na Bw Crump kwa pamoja walisema kuwa alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kiakili , na amekuwa akipata matibabu ya kiakili, lakini hakuweza kuendelea kumeza dawa hizo akiwa gerezani.

Familia ya Otieno ambayo ilitoka Kenya na kuhamia Marekani alipokuwa na umri wa miaka minne. Bw Otieno alikuwa na ndoto ya kuwa mwanamuziki na mwanamichezo, walisema, na alikuwa akiandika na kurekodi muziki wakat iwa muda wake wa ziada

 

 

 

 

 

.