Rais mpya wa Nigeria asafiri hadi Paris na London 'kupumzika'

Safari za mara kwa mara za rais mteule ng'ambo zinaendelea kuzusha uvumi kuhusu afya yake

Muhtasari

•Tunde Rahman, msemaji wa Bw Tinubu, katika taarifa yake Jumatano alisema rais mteule aliondoka nchini Jumanne.

•Alifanya safari kadhaa ambazo hazijatangazwa hadi Uingereza na Ufaransa kabla ya kampeni kuanza mnamo 2022.

Bola Tinubu, rais mteuel wa Nigeria.
Bola Tinubu, rais mteuel wa Nigeria.
Image: Reuters

Rais mteule wa Nigeria Bola Tinubu amesafiri hadi Ufaransa na Uingereza "kupumzika" na kupanga mpango wa mpito kabla ya kuapishwa kwake tarehe 29 Mei.

Tunde Rahman, msemaji wa Bw Tinubu, katika taarifa yake Jumatano alisema rais mteule aliondoka nchini Jumanne.

Kulingana na Bw Rahman, rais mteule baadaye ataadhimisha Hijja nchini Saudi Arabia.

"Rais mteule aliamua kupumzika baada ya kampeni na msimu wa uchaguzi wenye shughuli nyingi kupumzika Paris na London, kujiandaa kwenda Saudi Arabia kwa Umrah (Hajj Ndogo) na mfungo wa Ramadhani unaoanza Alhamisi," Bw Rahman alisema.

Aliongeza kuwa Bw Tinubu anatarajiwa kurejea nchini "hivi karibuni".

Safari za mara kwa mara za rais mteule ng'ambo zinaendelea kuzusha uvumi kuhusu afya yake.

Alifanya safari kadhaa ambazo hazijatangazwa hadi Uingereza na Ufaransa kabla ya kampeni kuanza mnamo 2022.

Pia anakabiliwa na vita vya kisheria kuhusu ushindi wake katika uchaguzi wa rais wa mwezi uliopita.