Trump akamatwa na kushtakiwa kwa makosa 34 ya uhalifu

Trump amekana mashtaka 34 yanayohusiana na kughushi rekodi za biashara

Muhtasari

•Trump amekana mashtaka baada ya kushtakiwa kwa makosa 34 ya uhalifu, ikiwa ni pamoja na kughushi rekodi za biashara.

•Alionekana mtulivu alipokuwa akiingia ndani ya mahakama, akisimama kuupungia mkono umati.

Image: BBC

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amekana mashtaka baada ya kushtakiwa kwa makosa 34 ya uhalifu, ikiwa ni pamoja na kughushi rekodi za biashara.

Donald Trump aliondoka kwenye chumba cha mahakama huko Manhattan.Hakutoa maoni yoyote na kupuuza maswali kutoka kwa waandishi wa habari.

Alitarajiwa kurejea nyumbani kwake Florida, ambako inatarajiwa atazungumza baadaye.

Nini tunachojua kuhusu mashtaka dhidi ya Trump?

Haya hapa maelezo kuhusu mashtaka hayo 34:

  • Jalada la mahakama linasema rais huyo wa zamani "kwa nia ya kudanganya na nia ya kufanya uhalifu mwingine na usaidizi na kuficha makosa yake, alifanya na kusababisha kuweka kwa uwongo rekodi za biashara
  • Mashtaka dhidi ya Trump yote ni makosa ya daraja la E.Hiyo ndiyo aina ya chini kabisa ya makosa ya jinai huko New York na ina adhabu ya juu zaidi ya miaka minne kwa kila kosa.
  • Kughushi rekodi za biashara kwa kawaida hushtakiwa kama kosa
  • Ofisi ya wakili wa wilaya ya Manhattan inaongeza shtaka hilo kwa kudai kuwa kosa lilitendwa ili kuficha au kutenda uhalifu mwingine.
  • Trump amekana mashtaka yote