Muongozo kamili ya kutawazwa kwa Mfalme Charles III

Siku hiyo ya fahari na rasmi inagubikwa na tamaduni za kuanzia miaka zaidi ya 1,000- iliyopita.

Muhtasari

•Mamilioni ya watu kutoka kote nchini Uingereza na nje ya nchi wanajiandaa kusherehekea kutawazwa kwa Mfalme Charles III -sherehe inayojumuisha dini na tamasha.

•Ni chini tu ya watu 200, kati ya wanajeshi - wengi wao kutoka katika kikosi cha farasi au Sovereign's Escort of the Household Cavalry – ambao watashiriki katika maandamano kuelekea Westminster Abbey 

Image: BBC

Mamilioni ya watu kutoka kote nchini Uingereza na nje ya nchi wanajiandaa kusherehekea kutawazwa kwa Mfalme Charles III -sherehe inayojumuisha dini na tamasha.

Inafanyika katika Westminster Abbey tarehe 6 Mei na Mfalme ambaye atakuwa anatawazwa pamoja na Camilla, Queen Consort, atakuwa anavishwa taji kama Mfalme wa 40 kuongoza ufalme huo tangu 1066.

Siku hiyo ya fahari na rasmi itagubikwa na tamaduni za kuanzia miaka zaidi ya 1,000- iliyopita. Hivi ndivyo tunavyotarajia mambo yatakavyokuwa.

Sherehe rasmi zitaanza kwa msafara kutoka Buckingham Palace hadi Westminster Abbey huku maeneo ya kutaza tukio hili, yakiwa kwenye njia itakayofunguliwa saa kumi na mbili asubuhi kwa saa za Uingereza (06:00 BST).

Maeneo yatakayoweza kufikiwa na umma karibu na The Mall na Whitehall yatakuwa kwa yule atakayefika mapema , ndiye atakayehudumiwa wa kwanza ,ambapo watu watakuwa wakiongozwa kuelekea maeneo yenye skrini rasmi za kufuatilia tukio ya Hyde Park, Green Park na St James's Park wakati yatakapokuwa yamejaa.

Maeneo ya kuketi kwa ajili ya wageni waalikwa, wakiwemo wanajeshi wastaafu na wahudumu wa afya NHS, pamoja na wafanyakazi wa jamii yameandaliwa nje ya Buckingham Palace.

Ni chini tu ya watu 200, kati ya wanajeshi - wengi wao kutoka katika kikosi cha farasi au Sovereign's Escort of the Household Cavalry – ambao watashiriki katika maandamano kuelekea Westminster Abbey watakaoanza kukusanyika Jumamosi asubuhi.

Wanajeshi wengine 1,000 watajipanga njiani, lakini maandamano kwa ujumla yatakuwa madogo zaidi kuliko yale ya mwaka 1953 wakati familia za kifalme na waziri mkuu wa Jumuiya ya Madola walikuwa miongoni mwa washiriki.

Msafara kuanza

Msafara utaanzia Buckingham Palace na kuzunguka kwenye The Mall hadi Trafalgar Square, halafu yataelekea Whitehall na Mtaa wa Bunge -Parliament Street, kabla ya kurudi katika Parliament Square na Broad Sanctuary ili kufika kwenye lango kuu la Westminster Abbey.

Katika kuepuka kidogo utamaduni, Mfalme Charles na Queen Consort Camilla watakuwa na Kiti cha Jubilei ya taifa ya Almasi badala ya kile cha zamani, sio cha starehe , Kiti cha Kitaifa cha Dhahabu.

Image: BBC

Kuwasili Westminster Abbey

Maandamano yanatarajiwa kuwasili katika abbey muda mfupi kabla ya saa tano kwa saa za eneo, huku ikitarajiwa inatarajiwa kuwa Mfalme kuwa anaweza kuvaa magwanda ya jeshi badala ya mavazi ya kitamaduni na soksi ndefe zilizovaliwa na wafalme kabla yake.

Image: bbc

Mfalme anaweza kuvaa sare za jeshi kama ile aliyoivaa wakati wa ibada ya mazishi ya mama yake mwaka jana, wakati baba yake George VI alivaa buti ndefu zinazofika usawa wa magoti (breeches) na soksi ndefu katika siku ya kutawazwa kwake

11:00

Mfalme Charles ataingia kupitia lango la Great West Door na kuendelea kupitia kwenye njia hiyo hadi atakapofika kwenye nafasi ya katikati katika abbey.

Sherehe inatarajiwa kuanza saa kuanza saa 5 za asubuhi (11:00 kwa saa za Uingereza) na zitatumbuizwa kwa muziki uliochaguliwa na Mfalme, huku miziki 12 mipya , mkiwemo ule wa Andrew Lloyd Webber, na muziki wa Waorthodox wa Ugiriki kwa ajili ya kumkumbuka yabbaba yake mfalme , Mwanamfalme Philip.

Mjukuu wa mfalme, Mwanamfalme George, atakua miongoni mwa kurasa za Westminster Abbey, pamoja na wajukuu wa Camilla, Lola, Eliza, Gus, Louis na Freddy.

Baadhi ya wale watakaoshiriki katika maandamano ndani ya abbey watabeba vito vya thamani mbele ya Mfalme, huku vingi kati ya vito hivyo vikiwa vimewekwa kwenye madhabahu hadi vitakapohitajika katika sherehe.

Regalia ni nini?

Image: BBC

Kulingana na wavuti wa ufalme, Uingereza ndio nchi pekee ya Ulaya ambayo bado inatumia regalia – alama za kifalme kama vile taji, fimbo la tufe ya dhahabu -katika kuwatawaza wafalme wake.

Vitu hivi vya mtu binafsi ni alama ya mbali mbali zinaonyesha huduma na waji kwa ufalme.

Charles atakabidhiwa tufe ya dhahabu au Orb, Fimbo ya enzi pamoja na msalaba, Fimbo ya enzi na njiwa na vitu vingine katika nyakati muhimu katika sherehe.

Na Camilla atakabidhiwa Fimbo ya Ufalme au Consort's Rod pamoja na Njiwa na Fimbo ya Kifalme ya Consort pamoja na Msalaba- kuakisi Fimbo ya Mfalme.

Hatua ya kwanza: Kutambuliwa

Mfalme Charles atawasilishwa kwa "watu" - utamaduni ulioanza zamani tangu nyakati za Anglo-Saxon.

kiwa amesimama kando ya kiti cha kutawaza kilichodumu kwa miaka 700, Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby atageuka kila upande wa abbey ana kumtangaza "bila shaka Mfalme " kabla ya kulitaka kongamano lionyeshe heshima zake na huduma.

Maelezo zaidi kuhusu kutawazwa

Kongamano litapaza sauti"Mungu Muokoe Mfalme!" na tarumbeta zitalia baada ya kila utambuzi.

Kiti cha kutawazwa, ambacho pia kinaitwa St Edward's Chair au King Edward's Chair, kinaaminiwa kuwa ndio kifaa cha samani cha zamani zaidi nchini Uingereza ambacho bado kinatumika kwa lengo lake asilia. Jumla ya wafalme 26 wametawazwa katika kiti hicho.

Asilia kilitengenezwa kwa agizo la Mfalme wa England, Edward I kufunga jiwe la Hatima, ambalo lilichukuliwa kutoka karibu na Scone katika Uskochi.

Jiwe – ambayo ni alama ya kale ya ufalme wa Uskochi – lilirejeshwa uskochi mwaka 1996 lakini litahamishiwa tena London kwa ajili ya kutumiwa katika ibada.

Wakati wa kutawazwa, kiti maalumu huwekwa katikati ya sakafu ya kihistoria "Cosmati pavement", mbele ya kikitazama katika Madhabahu ya Juu- High Altar, kusisitizia umuhimu wa kiasili wa dini wa sherehe.

Image: bbc

Hatua ya pili : Kiapo

Askofu Mkuu wa Canterbury atamtaka Mfalme Charles kuthibitisha kwamba ataheshimu sheria na kanisa la England wakati wa enzi yake, kabla ya Mfalme kuweka mkono wake kwenye Injiri Takatibu na Kula Kiapo cha Kutawazwa – sharti kisheria.

Mfalme Charles anaweza kuongeza baadhi ya maneno ili kukubali Imani nyingi zinazokubalika nchini Uingereza, ingawa huenda hili halitakuwa sehemu ya kiapo chenyewe, na halijathibitishwa.

Hatua ya tatu : Upako

Vazi la sherehe la mfalme ya litaondolewa na ataketi katika kiti cha kutawazwa ili kupakwa upako, kusisitizia hadhi ya kiroho ya enzi yake, akiwa pia ndiye mkuu wa Kanisa la England.

Askofu mkuu atamwaga mafuta maalumu kutoka kwenye Ampulla – bilauli ya dhahabu - kwenye kijiko cha kutawaza- Coronation Spoon, kabla ya kumuweka wakfu Mfalme kwa njia ya msalaba kwenye kicha chake, kifua na mikono.

Ampulla ilitengenezwa kwa ajili ya kutawazwa kwa Charles II, lakini muundo wake ulibadilishwa na kuwa katika muundo wake asilia unaofanana na ule ambao Bikra Maria alimuonyesha Mtakatifu Thomas karne ya 12 na kumpatia ishara ya mwewe dhahabu ambayo hutumiwa wakati Mfalme wa England anapopewa upako .

Kijiko cha Kutawazwa ni cha kale zaidi, kwani kilinusurika na uharibifu wa vito vya Kifalme baada ya Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya England.

Mafuta yenyewe yalitengenezwa kwa ajili ya kutawazwa huvunwa kutoka kwenye miti miwili ya mizeituni katika Mlima wa Mizeituni katika Jerusalem, na kuwekwa wakfu katika ibada maalum ya Kanisa Church la Holy Sepulchre lililopo mjini.

Kitambaa maalum kinachofahamika kama canopy kinaweza kushikiliwa kwenye kiti ili kumficha Mfalme asionekane na watu, kwasababu hii inachukuliwa kama sehemu ya wakfu zaidi ya ibada.

Hatua ya nne: Kutawazwa

Muda wa kuvikwa taji - wakati Mfalme atakapovaa Taji la St Edward kwa muda pekee katika maisha yake.

Taji huitwa jina baada awali lilipewa jina la falme wa Anglo-Saxon na mtakatifu , Edward the Confessor, na linasemekana kuwa limekuwa likitumiwa katika sherehe za kutawazwa baada ya 1220 hadi Cromwell alipolivunja.

Lilitengenezwa kwa ajili ya Mfalme Charles II, ambaye alitaka taji linalofanana na lile lililovaliwa na Edward lakini pia kubwa zaidi.

Mfalme Charles III atakuwa ni mfalme wa saa kulivaa baada ya Charles II, James II, William III, George V, George VI na Elizabeth II – ambaye mara ya mwisho alilivaa alipotawazwa mwaka 1953.

Kwanza Mfalme atakabidhiwa vitu mbali mbali mkiwemo Tufe ya Enzi , Pete ya Kutawazwa, fimbo ya enzi yenye msalaba na Fimbo ya enzi yenye Njiwa.

Halafu askofu mkuu ataweka taji la St Edward kwenye kichwa cha Mfalme na tarumbeta zitapigwa na mizinga ya bunduki itafyatuliwa kote nchini Uingereza.

Mizinga itafyatuliwa kwa awamu 62 katika mnara wa London - Tower of London, w huku mizinga sita ya bunduki ikipigwa kutoka kwenye kikosi cha farasi -Horse Guards Parade. Mizinga itafyatuliwa kwa awamu 21 katika maeneo mengine 11 zaidi kote nchini Uingereza, ikiwa ni pamoja na Edinburgh, Cardiff na Belfast, na katika meli za vikosi vya wanamaji vya Uingereza vilivyotumwa katika maeneo mbali mbali.

Hatua ya tano: Kuvikwa taji

Sehemu ya mwisho ya sherehe itakuwa ni kushuhudiwa kwa Mfalme akila kiapo. Anaweza hata kuapishwa na askofu mkuu, maaskofu na wenzake katika ufalme.

Kitamaduni, kutoa heshima kwa ufalme na wenzake kungefanyika kwa kupiga magoti mbele ya mfalme mpya, kula kiapo kwake na kuubusu mkono wake wa kulia

Hatahivyo, inadhaniwa kuwa Mwanamfalme William atakuwa ndiye Mfalme wa Duke ambaye atatoa heshima kwa Mfalme Charles.

Mke wa Mfalme

Baada ya tukio hilo, Malkia Camilla atapakwa mafuta, kuvishwa tajin a kusimikwa katika sherehe rahisi zaidi – ingawa hatalazimika kula kiapo.

Atavishwa taji la Malkia Mary - ambalo asilia lilitengenezwa kwa ajili ya kutawazwa kwa malkia Mary pamoja na George V – lakini linabadilishwa kuondoa baadhi ya nakshi na kuwekewa nambari za kirumi III, IV na V za almasi.

Kuondoka

Mfalme na Queen Consort wataondoka kutoka kwenye enzi viti vyao vya enzi na kuna uwezekano mkubwa kuwa wataingia katika kanisa dogo la St Edward's Chapel – hapa Charles ataondoa St Taji la Edward na kuvaa Taji la taifa la Kifalme kabla ya kujiunga na maandamano nje ya abbey a huku wimbo wa taifa ukichezwa.

Mfalme na Queen Consort hatimaye atarejea katika Buckingham Palace kupitia barabara ya nyuma ambayo waliitumia kuja, wakati huu wakisafiri katika gari dogo la magurudumu lililodumu kwa miaka 260 - Gold State Coach ambayo imekuwa ikitumiwa katika kuapishwa tangu kutawazwa kwa William IV mwaka 1831.

Ripoti zinasema watoto watatu wa Mwanamfalme wa Wales, mwanamfalme George na Louis na Bintimfalme Charlotte, watajiunga na maandamano pamoja na wazazi wao, wakiketi nyuma katika gari maalum la magurudumu la kifalme linalofahamika kama - Gold State Coach.

Karibu, wanajeshi 4,000 wa kikosi cha Uingereza watashiriki katika kile ambacho wizara ya ulinzi imekiita operesheni kubwa zaidi ya kijeshi ya aina yake kuwahi kushuhudiwa katika kizazi hiki.

Watajiunga na wawakilishi kutoka nchi za Jumuiya ya Madola na Maeneo ya Uingereza yaliyo nje yake.

Na kikosi cha Ufalme wa Uingereza, the Royal British Legion kitatoa walinzi imara 100-wa gwaride la heshima kwa ajili ya kushiriki maandamano ya kuelekea kwenye medani ya bunge- Parliament Square.

Njia hiyo ina umbali wa maili 1.42 (km 2.29) kutoka abbey ukitoka kwenye viwanja vya kasri. Mfalme na malkia watapokea saluti ya kifalme- Royal Salute na kushangiliwa mara tatu na wanajeshi ambao watakuwa katika gwaride.

Mwaka 1953, njia ilikuwa na urefu wa zaidi ya maili nne na ilichukua dakika 45 kwa maa to ndamano kamili yaliyopitia kituo kimoja.

Kupaa kwa ndege juu ya Kasri ya Buckingham Palace

Umekuwa ni utamaduni tangu kutawazwa kwa Edward VII mwaka 1902 kwa mfalme mpya fkusalimia umati kutoka kwenye the Mall akiwa kwenye roshani ya Buckingham Palace - Malkia alikuwa na mama yake, watoto na dada miongoni mwa wanafamilia wa Ufalme alipokuwa akitazama maonyesho ya ndege zinazopaa juu yake angani , ambayo yalishirikisha mamia ya ndege mwaka 1953.

Umekuwa ni utamaduni tangu kutawazwa kwa Edward VII mnamo mwaka 1902 kwa mfalme mpya kusalimia umati mbali mbali wa watu kwenye The Mall kutoka kwenye roshani ya Buckingham Palace -Malkia aliungana na mama yake, watoto na dada yake miongoni mwa watu wa familia ya Kifalme wakati akitazama mamia ya ndege zikipaa juu katika mwaka 1953.

Imeandikwa na kuandaliwa na Chris Clayton, kufanyiwa kazi ya ziada Lilly Huynh na Zoe Bartholomew, naelezo ya picha na Jenny Law