Mshambulizi aua watu 8 kwa risasi dukani wakiwemo watoto

Takriban watu saba wanatibiwa hospitalini, watatu kati yao ni wakiwa mahututi

Muhtasari

•Mtu mwenye silaha amewauwa watu wanane waliokuwa wakifanya ununuzi katika moja ya maduka makubwa kaskazini mwa Dallas, Texas.

•Watu walioshambuliwa wanatajwa kuwa na umri kati ya miaka 5 hadi 51, kulingana na msemaji wa hospitali.

Image: BBC

Mtu mwenye silaha amewashambulia kwa risasi na kuwauwa watu wanane waliokuwa wakifanya ununuzi katika moja ya maduka makubwa kaskazini mwa Dallas, Texas.

Mamia ya watu waliondolewa kutoka kwa maduka ya Allen Premium Outlets huku watu walioshuhudia wakieleza mtu huyo alikuwa akiwafyatulia risasi wapita njia kiholela.

Afisa wa polisi aliyekuwa karibu na eneo la tukio alimuua mtu huyo mwenye bunduki baada ya kusikia milio ya risasi. Baadhi ya walioshambuliwa wanaripotiwa kuwa watoto.

Takriban watu saba wanatibiwa hospitalini, watatu kati yao ni wakiwa mahututi. Mkuu wa Zimamoto Allen Jonathan Boyd alisema watu saba - ikiwa ni pamoja na mshambuliaji huyo - walitangazwa kufariki katika eneo la tukio na wawili walikufa baadaye hospitalini.

Afisa usalama katika jengo la maduka "alisikia milio ya risasi, akaenda kwenye eneo la tukio, na kufanikiwa kumzuia mshukiwa," Mkuu wa Polisi wa Allen Brian Harvey alisema.

Watu walioshambuliwa wanatajwa kuwa na umri kati ya miaka 5 hadi 51, kulingana na msemaji wa hospitali.