Andrew Tate ashtakiwa kwa ubakaji na biashara ya kusafirisha binadamu

Mnamo tarehe 31 Machi, walihamishwa kutoka kizuizini hadi kizuizi cha nyumbani kufuatia uamuzi wa hakimu wa Romania.

Muhtasari
  • Kaka yake Tristan na washirika wake wawili pia wameshtakiwa. Wote wamekanusha madai hayo.

Mshawishi wa mitandao ya kijamii mwenye utata Andrew Tate ameshtakiwa nchini Romania kwa ubakaji, ulanguzi wa binadamu na kuunda kikundi cha uhalifu uliopangwa ili kuwadhulumu wanawake kingono.

Kaka yake Tristan na washirika wake wawili pia wameshtakiwa. Wote wamekanusha madai hayo.

Akina Tate walikamatwa kwa mara ya kwanza nyumbani kwao Bucharest mnamo 2022.

Mnamo tarehe 31 Machi, walihamishwa kutoka kizuizini hadi kizuizi cha nyumbani kufuatia uamuzi wa hakimu wa Romania.

Shtaka lililowekwa katika mahakama ya Bucharest linasema kuwa washtakiwa hao wanne waliunda kundi la uhalifu lililopangwa mwaka 2021 kufanya biashara ya binadamu nchini Romania, lakini pia katika nchi nyingine zikiwemo Marekani na Uingereza.

Inataja waathiriwa saba ambao inasema waliajiriwa na ndugu wa Tate kupitia ahadi za uwongo za mapenzi na ndoa.

Kesi hiyo inatarajiwa kuchukua miaka kadhaa.