Shambulio la shule Uganda: Watu 20 wakamatwa kuhusiana na mauaji

Mwalimu mkuu na mkurugenzi wa shule ni miongoni mwa waliozuiliwa.

Muhtasari

•Polisi nchini Uganda wanasema wamewakamata watu 20 wanaoshukiwa kushirikiana na wanamgambo wa Kiislamu kushambulia shule Ijumaa iliyopita.

Image: BBC

Polisi nchini Uganda wanasema wamewakamata watu 20 wanaoshukiwa kushirikiana na wanamgambo wa Kiislamu wanaoaminika kushambulia shule Ijumaa iliyopita.

Mwalimu mkuu na mkurugenzi wa shule ni miongoni mwa waliozuiliwa.

Watu 42 - wengi wao wakiwa wanafunzi - waliuawa katika Shule ya Sekondari ya Lhubiriha huko Mpondwe magharibi mwa Uganda.

Wengi walichomwa hadi kufa katika bweni lao.

Jeshi la Uganda bado linawasaka wapiganaji wa Allied Democratic Forces (ADF), ambao wameripotiwa kurejea tena kwenye mpaka wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako ndiko makazi yao.