Mwanaume atakayesuka nywele Zanzibar kufungwa jela miezi 6

Serikali ya Zanzibar imesema ni kosa kisheria mwanaume kuingia au kuishi viziwani Zanzibar akiwa amesuka nywele.

Muhtasari

•''Kwa mujibu wa sheria zetu ukikutwa utatozwa faini ya milioni moja za kitanzania ambayo ni zaidi ya dola 400 za kimarekani  (Ksh 56,500)  au kufungwa jela miezi sita au adhabu zote kwa pamoja,” serikali imesema.

•.Dkt Omar amesema vijana wengi visiwani humo wamekuwa na hulka ya kusuka nywele kinyume na taratibu za wazanzibar.

Image: BBC

Serikali ya Zanzibar imesema ni kosa kisheria mwanaume kuingia au kuishi viziwani Zanzibar akiwa amesuka nywele.

''Kwa mujibu wa sheria zetu ukikutwa utatozwa faini ya milioni moja za kitanzania ambayo ni zaidi ya dola 400 za kimarekani  (Ksh 56,500)  au kufungwa jela miezi sita au adhabu zote kwa pamoja,” imeeleza Serikali ya Zanzibar.

Akizungumza na BBC, Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar, Dkt Omar Adam amesema serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imeanza operesheni ya kukamata wanaume wote waliosuka nywele ikiwa ni utekelezaji wa sheria inayokataza wanaume kusuka nywele ili kulinda maadili na tamaduni za Zanzibar.

Dkt Omar amesema vijana wengi visiwani humo wamekuwa na hulka ya kusuka nywele kinyume na taratibu za wazanzibar.

Alisema,” Sifahamu kama kuna mzee yoyote hapa Zanzibar ambaye atamchukua mwanae wa kiume halafu ampeleke saluni kusuka nywele. Huu si utamaduni wa Zanzibar na sisi kama wasimamia sheria lazima tuzuie hili.”