Mzozo wa Israel na Hamas: Haya ndiyo yanayojiri hivi punde

haya hapa ni baadhi ya matukio muhimu yaliyojiri saa chache zilizopita.

Muhtasari

•Kuna "milio ya risasi na milipuko ya mara kwa mara" katika eneo karibu na hospitali, kulingana na mkuu wa WHO Tedros Adhanom.

Image: BBC

Ikiwa unajiunga nasi, au unahitaji muhtasari, haya hapa ni baadhi ya matukio muhimu yaliyojiri saa chache zilizopita.

  • Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linasema hospitali ya Al-Shifa katika Jiji la Gaza "haifanyi kazi kama hospitali tena"
  • Kuna "milio ya risasi na milipuko ya mara kwa mara" katika eneo karibu na hospitali, kulingana na mkuu wa WHO Tedros Adhanom, ambayo "imezidisha hali ambayo tayari ni mbaya"
  • Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas inasema zaidi ya watu 2,000 wako ndani ya Al -Shifa, wakiwemo wagonjwa, wahudumu wa afya na waliokimbia makazi yao.
  • Jeshi la Israel limekariri kuwa ''liko tayari kusaidia'' kuwahamisha watoto kadhaa kutoka hospitalini - lakini linakanusha kugonga hospitali wakati wa mapigano na Hamas.
  • Madaktari wa Al-Shifa wanasema wanahofia kwamba watoto 36 waliosalia wanaohitaji matibabu ya uangalizi mkubwa wanaweza kufa huku shirika la misaada la Medical Aid kwa Wapalestina likisema bila ambulensi, vifaa muhimu au hospitali ya kuwahamisha watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, "hakuna dalili ya jinsi ili linaweza kufanyika kwa usalama''
  • Kwingineko, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema wakati wa mahojiano na mtandao wa NBC wa Marekani kwamba '' kunaweza kuwa '' makubaliano ya kuwaachilia mateka wa israel waliosalia Gaza - lakini hakutoa maelezo yoyote.