Watu 3 wakamatwa kwa ponografia ya watoto na ngono dhidi ya wanyama

Wanaume watatu wanaotuhumiwa kuwadhulumu kingono watoto watatu na mbwa wamekamatwa.

Muhtasari

•Washukiwa hao ni pamoja na raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 63 ambaye alikuwa nchini kinyume cha sheria.

•Polisi wanasema operesheni ya "kufumua mtandao wa wanyanyasaji watoto kingono" bado inaendelea.

Image: BBC

Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini imesema imewakamata wanaume watatu wanaotuhumiwa kuwadhulumu kingono watoto watatu na mbwa katika operesheni iliyoendeshwa kwa usaidizi wa Idara ya Usalama wa Ndani ya Marekani wiki jana.

"Kutokana na operesheni hizi, watoto watatu wa Afrika Kusini ambao walitumiwa wakati wa kutenda makosa hayo walitambuliwa na mbwa aliokolewa," polisi walisema katika taarifa siku ya Jumanne.

Washukiwa hao ni pamoja na raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 63 ambaye alikuwa nchini kinyume cha sheria.

Polisi wanasema atashtakiwa kwa makosa ya ngono dhidi ya wanyama, malezi ya watoto na makosa kadhaa yanayohusiana na ponografia ya watoto, ikiwa ni pamoja na kutengeneza na kusambaza ponografia ya watoto.

Mshukiwa wa pili na wa tatu, wote wakiwa na umri wa miaka 43 kutoka Afrika Kusini, pia watashtakiwa kwa makosa kadhaa ya ponografia ya watoto, polisi wanasema.

Polisi waliongeza kuwa washukiwa hao walifika mahakamani siku ya Jumatatu lakini kesi zao "ziliahirishwa kwa uchunguzi zaidi na maombi ya kuachiliwa kwa dhamana".

Polisi wanasema operesheni ya "kufumua mtandao wa wanyanyasaji watoto kingono" bado inaendelea.