Kitendo cha ujambazi kilichofanywa na mwanamke kilichowashangaza hata majaji

Steenkamp tayari amekiri mashtaka 336 ya uhalifu.

Muhtasari

•Hildegard Steenkamp amekuwa akiiba pesa hizi kwa miaka 13, na kuziiba kutoka kwa kampuni ambayo alikuwa mhasibu ya huduma ya afya iliyopo Gauteng.

•Hakimu alisema hajawahi kushughulikia kesi inayohusu wizi wa pesa, inayohusisha mtu mmoja pekee kwa kiasi hicho cha pesa.

Image: BBC

Mwanamke wa Afrika Kusini alipatikana na hatia ya kuiba dola milioni 28 kutoka kwa kampuni aliyoifanyia kazi, na alihukumiwa kifungo cha miaka 50 jela.

Hildegard Steenkamp amekuwa akiiba pesa hizi kwa miaka 13, na kuziiba kutoka kwa kampuni ambayo alikuwa mhasibu ya huduma ya afya iliyopo Gauteng.

Steenkamp tayari amekiri mashtaka 336 ya uhalifu.

Alifika mbele ya hakimu ambaye alisema hajawahi kushughulikia kesi inayohusu wizi wa pesa, inayohusisha mtu mmoja pekee kwa kiasi hicho cha pesa

Jaji Phillip Venter alielezea kushtushwa kwake na kitendo hiki akisema "kuelewa kuwa mfanyakazi mmoja aliiba pesa nyingi kiasi hiki kutoka kwa kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi ni jambo la ajabu," alisema hakimu.

Mwanamke huyo alijitetea kwamba alilazimika kufanya hivyo baada ya kudhulumiwa na mume wake aliyefariki ambaye alimlazimisha kufanya kitendo hiki Lakini Jaji Venter hakukubaliana na hoja hiyo akasema kwamba alifanya hivyo peke yake.

Wachunguzi waligundua kuwa Steenkamp alitumia pesa hizo kufadhili maisha yake ya kifahari ya kamari, kununua vito vya thamani na kusafiri.

Moja ya matumizi ya pesa hizo ni $263,000 ambazo alichezesha kamari kwa usiku mmoja.

Mahakama pia iliambiwa kuwa Steenkamp alitumia karibu $1.6m kwa safari zake za kimataifa na alitembelea Dubai mara kwa mara.

Alifanya kazi katika kampuni hiyo kutoka 2004 hadi 2017, kabla ya kujiuzulu.