Putin kuwania muhula wa tano kama rais wa Urusi

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema atawania tena muhula wa tano madarakani.

Muhtasari

•Kiongozi huyoNmwenye umri miaka 71 tayari amekuwa madarakani nchini Urusi kwa muda mrefu kuliko mtawala yeyote tangu Josef Stalin.

Image: BBC

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema atawania tena muhula wa tano madarakani.

Alizungumza kuhusu nia yake wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa washiriki katika vita nchini Ukraine.

Inakuja siku moja baada ya maafisa kuweka tarehe 15-17 Machi 2024 kama tarehe za uchaguzi wa urais.

Kuchaguliwa tena kwa Bw Putin kunaonekana kuwa jambo lisiloepukika, huku upinzani ukikaribia kutokomeana vyombo vya habari vya Urusi vikiwachini ya udhibiti wake.

Kiongozi huyoNmwenye umri miaka 71 tayari amekuwa madarakani nchini Urusi kwa muda mrefu kuliko mtawala yeyote tangu Josef Stalin. Muhula mpya utamfanya aendelee kuwa rais hadi 2030.

Siku ya Alhamisi, baraza la juu la bunge la Urusi, Baraza la Shirikisho, lilitangaza uchaguzi huo. Muda mfupi baadaye, tume ya uchaguzi nchini humo ilisema kuwa utafanyika kwa muda wa siku tatu, kuanzia tarehe 15-17 Machi.

Kufuatia tangazo hilo, msemaji rasmi wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, alisema kuwa idadi "ya kushangaza"ya watu wanamtaka Bw Putin aendelee kuwa kiongozi.

Hakuchukua muda mrefu kuweka nia yake wazi.

Bw Putin alizungumza kwenye mkutano usio rasmi baada ya sherehe katika Ikulu ya Kremlin ya kuwatunuku mashujaa wa vita wa Ukraine ‘nishani ya shujaa wa Urusi’.