Rais wa DRC Tshisekedi amlinganisha Kagame wa Rwanda na Hitler

Kinshasa inasema M23 inaungwa mkono na Rwanda, ingawa Kigali imekuwa kikikanusha madai hayo.

Muhtasari

•Tshisekedialimlinganisha Kagame na Adolf Hitler wakati wa hotuba yake kuhusu kampeni katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo lililokumbwa na mzozo.

Image: BBC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Felix Tshisekedi Ijumaa alimlinganisha mwenzake wa Rwanda na Adolf Hitler wakati wa hotuba yake kuhusu kampeni katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo lililokumbwa na mzozo.

Mashariki mwa DRC imekumbwa na miongo kadhaa ya ghasia zisizokwisha za makundi ya waasi, wakiwemo waasi wa M23 wanaoongozwa na Watutsi ambao wameteka maeneo mengi ya ardhi tangu kuanza mashambulizi mwishoni mwa 2021.

Kinshasa, pamoja na mataifa kadhaa ya Magharibi yakiwemo Marekani na Ufaransa, yanasema M23 inaungwa mkono na Rwanda, ingawa Kigali imekuwa kikikanusha madai hayo.

"Nitazungumza na Rais wa Rwanda Paul Kagame na kumwambia hivi: kwa kuwa alitaka kuwa na tabia kama Adolf Hitler kwa kuwa na malengo ya kujitanua (nchini DRC), ninaahidi ataishia kama Adolf Hitler," Tshisekedi aliuambia umati wa watu waliokuwa wakishangilia. katika mkutano wa hadhara Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini.