Mbongeni Ngema: Nguli wa sanaa wa Afrika Kusini aombolezwa

Kazi zake "zilionyesha roho ya upinzani" wakati wa utawala wa wazungu wachache, familia yake ilisema

Muhtasari
  • Alipata umaarufu wa kimataifa katika miaka ya 1980 kwa tamthilia zilizosawiri maisha ya watu weusi chini ya mfumo wa ubaguzi wa rangi wa ubaguzi wa rangi.

Salamu za rambirambi zimeendelea kutolewa kufuatia kifo cha mtunzi wa maigizo wa Afrika Kusini Mbongeni Ngema aliyefariki katika ajali ya gari akiwa na umri wa miaka 68.

Alipata umaarufu wa kimataifa katika miaka ya 1980 kwa tamthilia zilizosawiri maisha ya watu weusi chini ya mfumo wa ubaguzi wa rangi wa ubaguzi wa rangi.

Kazi zake "zilionyesha roho ya upinzani" wakati wa utawala wa wazungu wachache, familia yake ilisema

Ngema alijulikana zaidi kwa muziki wake Sarafina!, ambao baadaye ulibadilishwa kuwa filamu iliyoigizwa na Whoopi Goldberg.

Rais Cyril Ramaphosa aliongoza taifa kumuomboleza mtunzi wa maigizo na mwelekezajii wa tamthilia

"Masimulizi ya ustadi wa Ngema ya mapambano yetu ya ukombozi yaliheshimu ubinadamu wa Waafrika Kusini waliokandamizwa" na "kufichua unyama" wa utawala wa kibaguzi, kiongozi huyo wa Afrika Kusini alisema.

Alifariki katika ajali ya barabarani Jumatano jioni alipokuwa akirejea kutoka mazishini katika mji wa Lusikisiki lililopo jimbo la Eastern Cape.

Zaidi ya watu 700 wamefariki katika ajali za barabarani nchini Afrika Kusini tangu mwanzoni mwa mwezi Disemba.