Aliyehukumiwa miaka 30 jela kwa kushindwa kutunza mimba aachiliwa baada ya miaka 9

Mama huyo alijifungua kijusi ambacho hakikuwa kimetimia miezi 9 na kuwekwa kwenye incubator lakini kikafa saa 72 baadae, na hivyo kupelekea mamlaka kumfungulia mashtaka ya utelekezi.

Muhtasari

• El Salvador ina moja ya marufuku ya kikatili zaidi ya utoaji mimba katika Amerika, ambayo wakosoaji wanasema inaenea kwa wanawake wanaopata mimba na kuzaa watoto waliokufa.

 
• Wanawake wengi wamehukumiwa miongo kadhaa jela kwa tuhuma za kuua watoto wao.

Mwanamke mjamzito
Mwanamke mjamzito
Image: Maktaba

Mwanamke mmoja nchini El Salvador aliyehukumiwa miaka 30 jela mnamo mwaka 2015 kwa tuhuma za kushindwa kutunza mimba ameachiliwa huru baada ya rufaa yake kufaulu mahakamani.

Kwa mujibu wa AFP, Mwanamke huyo ambaye alimtajwa tu kama Lilian, alifungwa jela chini ya sheria kali ambazo kundi la wanawake lilisema Jumatano ilisababisha 'kuharamishwa kwa uzazi.'

Lilian alizungumza na vyombo vya habari Jumatano kwa mara ya kwanza tangu kuachiliwa kwake mwezi Desemba kutoka kifungo cha miaka 30 jela, na kutoa wito kwa watu nchini humo kuacha kuwashutumu wanawake wanaopatwa na dharura ya uzazi.

"Kuridhika ni kubwa sana kwa sababu licha ya kupitia mchakato mrefu, kutokuwa na hatia kumeweza kuthibitishwa," kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 aliliambia shirika la habari la AFP.

Mnamo 2015, Lilian alijifungua katika hospitali ya umma magharibi mwa El Salvador, lakini mtoto wake wa kike alipata matatizo, aliwekwa ndani ya incubator na kufariki saa 72 baadaye, wakili wake Abigail Cortez aliambia AFP.

Alifunguliwa mashitaka ya 'mauaji ya kupindukia' baada ya kushtakiwa kwa 'kutelekeza na kupuuza,' huku waendesha mashitaka wakisema kuwa ameshindwa kutunza kijusi alipokuwa mjamzito.

Alikuwa mwanamke wa mwisho bado kufungwa kwa mashtaka kama haya, kulingana na vikundi viwili vya haki za kiraia. Wengine bado wanakabiliwa na kesi za kimahakama.

Mnamo 2023, mahakama ilikagua hukumu hiyo na kuamuru aachiliwe.

Hakimu alimwachilia Lillian kwa misingi kwamba yeye na bintiye walikuwa katika hali hatarishi hospitalini wakati matukio hayo yalipotokea, makundi hayo yalisema.

El Salvador ina moja ya marufuku ya kikatili zaidi ya utoaji mimba katika Amerika, ambayo wakosoaji wanasema inaenea kwa wanawake wanaopata mimba na kuzaa watoto waliokufa.

Wanawake wengi wamehukumiwa miongo kadhaa jela kwa tuhuma za kuua watoto wao.

 

Idadi kubwa ya watu nchini humo ni Wakatoliki wa Roma au Wainjilisti - Wakristo wanaoamini kwamba maisha huanza wakati mimba inatungwa.