Saudi Arabia kufungua duka la kwanza la pombe baada ya zaidi ya miaka 70

Maafisa wa Saudi walisema duka hilo litakabiliana na "biashara haramu ya pombe"

Muhtasari

•Wateja wa mkahawa huo watakuwa wafanyakazi wa balozi, ambao kwa miaka mingi wameagiza pombe kutoka nje.

•Watumiaji wataruhusiwa kunywa ‘pointi’ 240 za pombe kwa mwezi.

Image: BBC
Image: BBC

Saudi Arabia imesema itafungua duka la pombe kwa wahamiaji maalum wasio Waislamu, mjini Riyadh, likiwa la kwanza kufunguliwa kwa zaidi ya miaka 70.

Wateja wa mkahawa huo watakuwa wafanyakazi wa balozi, ambao kwa miaka mingi wameagiza pombe kutoka nje katika vifurushi rasmi vilivyofungwa vinavyojulikana kama mifuko ya kidiplomasia.

Maafisa wa Saudi walisema duka hilo litakabiliana na "biashara haramu ya pombe".

Marufuku ya kuuza pombe imekuwa sheria tangu 1952, baada ya mmoja wa watoto wa kiume wa Mfalme Abdulaziz ambaye alikuwa amekunywa hadi kulewa kumuua kwa kumpiga risasi mwanadiplomasia wa Uingereza.

Duka hilo jipya litakuwa katika eneo linalopendwa sana na wanadiplomasia hao magharibi mwa katikati ya jiji, kulingana na waraka ulioonekana na mashirika ya habari ya AFP na Reuters.

Chanzo kinachofahamu mipango hiyo kiliiambia Reuters kuwa duka hilo lilitarajiwa kufunguliwa ndani ya wiki chache. Hatahivyo kutakuwa na masharti:

  • • Wajumbe wenye kiu watahitaji kujiandikisha kabla na kupokea kibali kutoka kwa serikali
  • • Hakuna aliye na umri wa chini ya miaka 21 atakayeruhusiwa dukani na "mavazi yanayofaa yanahitajika" wakati wowote ndani
  • • Wanywaji hawataweza kutuma wakala, kama vile dereva
  • • Masharti ya kila mwezi yatatekelezwa, taarifa hiyo ilisema.

Hatahivyo - kulingana na waraka ulioonekana na AFP – masharti hayo hayatakuwa makali.

Watumiaji wataruhusiwa kunywa ‘pointi’ 240 za pombe kwa mwezi. Lita moja ya vinywaji vikali itakuwa na thamani ya pointi sita, lita moja ya divai pointi tatu na lita moja ya bia pointi moja.

Pia hakuna mapendekezo kwamba wateja wataongezwa na kuorodhesha wageni "wa kawaida" .

Chini ya sheria ya sasa ya Saudia, adhabu za unywaji pombe zinaweza kujumuisha faini, kifungo cha jela, kuchapwa viboko hadharani na kufukuzwa nchini kwa wageni ambao hawajaidhinishwa.

Hati hiyo pia ilisema mamlaka inapanga "mfumo mpya wa udhibiti" ambao pia utaruhusu "kiasi maalum" cha pombe kuletwa na wanadiplomasia "kukomesha... ubadilishanaji usiodhibitiwa wa bidhaa kama hizo", iliongeza.

Kwa miaka mingi wafanyakazi wa kidiplomasia wamelazimika kutumia "pochi" zao, ambazo haziwe