Prince Harry awasili nyumbani kwa Mfalme Charles London

Safari ya Prince Harry nchini Uingereza ni kuonana na babake baada ya kugunduliwa kuwa na saratani.

Muhtasari

• Magari ya SUV mawili yenye rangi nyeusi yalionekana yakiingia kwenye VIP Windsor Suite ya Uwanja wa Ndege wa Heathrow.

Image: London News Pictures

Mwanamfalme Harry amewasili Uingereza baada ya kusafiri kutoka Marekani kwenda kumuona Mfalme.

Anaonekana kuwa aliingia katika Clarence House, nyumba ya London ya Mfalme Charles na Malkia Camilla.

Magari ya SUV mawili yenye rangi nyeusi yalionekana yakiingia kwenye VIP Windsor Suite ya Uwanja wa Ndege wa Heathrow mapema mchana wa leo, yilipigwa picha yakiwasili kwenye makao ya kifalme, shirika la habari la PA linaripoti.

Vyombo vya habari vingine vinachapisha picha inayoonyesha Duke wa Sussex akiwasili katika moja ya magari.

Safari ya Prince Harry nchini Uingereza ni kuonana na babake baada ya kugunduliwa kuwa na saratani.

Lakini hiyo haimaanishi kuwa mkutano wa familia utaleta pamoja Prince Harry na Prince William.

Kulingana na vyanzo, kwa sasa hakuna mpango wa ndugu hao kukutana wakati Prince Harry yuko London.