Ugiriki yahalalisha ndoa za watu wa jinsia moja

Waziri Mkuu Kyriakos Mitsotakis alisema sheria hiyo mpya "itakomesha kwa ujasiri ukosefu mkubwa wa usawa".

Muhtasari
  • Wapenzi wa jinsia moja sasa pia wataruhusiwa kisheria kuasili watoto baada ya kura ya Alhamisi ya 176-76 bungeni.
Image: Getty Images

Ugiriki imekuwa nchi ya kwanza yenye Wakristo wengi wa Orthodox kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja.

Wapenzi wa jinsia moja sasa pia wataruhusiwa kisheria kuasili watoto baada ya kura ya Alhamisi ya 176-76 bungeni.

Waziri Mkuu Kyriakos Mitsotakis alisema sheria hiyo mpya "itakomesha kwa ujasiri ukosefu mkubwa wa usawa".

Lakini imegawanya nchi, kwa upinzani mkali unaoongozwa na Kanisa la Othodoksi lenye nguvu. Wafuasi wake walifanya maandamano mjini Athens.

Wengi walionyesha mabango, walishikilia misalaba, walisoma sala na kuimba vifungu vya Biblia katika Syntagma Square katika mjii mkuu .

Mkuu wa Kanisa la Kiorthodoksi, Askofu Mkuu Ieronymos, alisema hatua hiyo "itaharibu mshikamano wa kijamii wa nchi hiyo".

Mswada huo ulihitaji wingi wa kura ili kupitishwa katika bunge hilo lenye wabunge 300.

Bw Mitsotakis alikuwa ameunga mkono mswada huo lakini akahitaji kuungwa mkono na vyama vya upinzani ili kuupitisha , huku wabunge kadhaa wa chama chake cha mrengo wa kulia wakipinga.