Papa adaiwa kutumia neno la dharau kwa wapenzi wa jinsi moja

Mashirika mengine ya habari ya Italia tangu wakati huo yamethibitisha maneno ya Papa yakinukuu vyanzo vingi.

Muhtasari
  • Ingawa ulikuwa ni mkutano wa ndani, maoni ya Papa yaliwasilishwa kwenye tovuti ya uchunguzi ya Italia, Dagospia.

Papa Francis ameripotiwa kutumia lugha ya dharau katika tukio ambalo linaweza kuwa na athari kubwa kuhusu mtazamo wake dhidi ya watu wa mapenzi ya jinsi moja unavyochukuliwa.

Alipoulizwa katika Baraza la Maaskofu wa Italia ikiwa wanaume wa jinsia moja wanapaswa kuruhusiwa sasa kufanya mafunzo ya ukasisi mradi tu wawe waseja, Papa Francis alisema hawapaswi.

Kisha anaaminika kuwa aliendelea kwa kusema kwa Kiitaliano kwamba tayari kulikuwa, katika Kanisa, wimbi la watu wengi wa mapenzi ya jinsi moja, ambayo inatafsiriwa kama maneno ya kukera sana.

Ingawa ulikuwa ni mkutano wa ndani, maoni ya Papa yaliwasilishwa kwenye tovuti ya uchunguzi ya Italia, Dagospia.

Mashirika mengine ya habari ya Italia tangu wakati huo yamethibitisha maneno ya Papa yakinukuu vyanzo vingi.

Kumekuwa na mshtuko kwa lugha iliyoripotiwa na Papa katika mkutano huu wa faragha, haswa kwani mara nyingi amekuwa akiongea hadharani kuwa na heshima kwa watu wa mapenzi ya jinsi moja.

Wafuasi wa Papa kwa muda mrefu wamekuwa wakibishana kwamba ingawa haki za watu hao zimebadilika sana katika Ukatoliki, Papa Francis amebadilisha mtazamo wa Kanisa.

Alipoulizwa kuhusu hilo mapema katika upapa wake, aligonga vichwa vya habari kwa kujibu, "Mimi ni nani nihukumu?"

Hivi karibuni alizua mshangao miongoni mwa wanamapokeo wa Kikatoliki kwa kusema makasisi wanapaswa kuwabariki wapenzi wa jinsia moja katika hali fulani na mara kwa mara amezungumzia kuhusu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja kukaribishwa Kanisani.