Goodluck Jonathan ana wasiwasi kuhusu utaratibu wa upigaji kura Afrika Kusini

"Tulichokuwa na wasiwasi nacho ni watu ambao hawajaenda katika majimbo yao kupiga kura," alisema.

Muhtasari

•Jonathan ambaye anaongoza timu ya waangalizi wa uchaguzi nchini Afrika Kusini, anasema ana wasiwasi kuhusu taratibu mpya za usajili nchini humo.

•"Elimu ya wapiga kura itahitaji kufanyika hata katika vituo vya kupigia kura, jambo ambalo litapunguza kasi ya mchakato huo," anasema.

Goodluck Jonathan
Image: BBC

Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan, ambaye anaongoza timu ya waangalizi wa uchaguzi nchini Afrika Kusini, anasema ana wasiwasi kuhusu taratibu mpya za usajili nchini humo.

"Tulichokuwa na wasiwasi nacho ni watu ambao hawajaenda katika majimbo yao kupiga kura," anaiambia BBC.

"Siku za nyuma, wapiga kura wangeweza kupiga kura zao katika miji mikubwa kama Pretoria, Johannesburg au Cape Town bila usumbufu mwingi.

"Hata hivyo, wakati huu, wapiga kura walihitaji kutuma maombi kwa tume ya uchaguzi kwa ajili ya kupangiwa kama walitaka kupiga kura nje ya jimbo lao lililosajiliwa."

Jonathan, ambaye aliongoza Nigeria kutoka 2010 hadi 2015, anasema wapiga kura wengi hawakuwa wamekamilisha mchakato huu, wakiamini wanaweza kupiga kura kama hapo awali.

Jonathan, mwenye umri wa miaka 66 pia anasema "mkanganyiko juu ya kuanzishwa kwa kura hiyo, hatua inayolenga kutoa fursa hata kwa wagombea binafsi kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Kusini, inaweza pia kuwa na athari.

"Elimu ya wapiga kura itahitaji kufanyika hata katika vituo vya kupigia kura, jambo ambalo litapunguza kasi ya mchakato huo," anasema.