Wanandoa wavua kisanduku chenye shilingi milioni 13 katika ziwa

Walipofungua ndani ya sanduku hilo walikuta limejaa noti za $100 zilizoharibiwa na maji.

Muhtasari

•James Kane na Barbie Agostini walirusha kamba ya kuvua yenye sumaku kwenye ziwa eneo la Queens siku ya Ijumaa na kuvuta kijisanduku.

•"Tulilitoa nje na ilikuwa ni rundo kubwa la mamia," aliongeza. "Hili ni rundo nene - zimelowa, zimeharibiwa sana," walisema.

Image: BBC

Wanandoa "wanaovua kwa sumaku" wanasema wamevuta kijisanduku kilichokuwa na wastani wa $100,000 (£78,000) (Sh13milioni) kutoka ziwa la New York.

James Kane na Barbie Agostini walirusha kamba ya kuvua yenye sumaku kwenye ziwa eneo la Queens siku ya Ijumaa na kuvuta kijisanduku.

Walipofungua ndani ya sanduku hilo walikuta limejaa noti za $100 zilizoharibiwa na maji.

Walisema polisi imewaambia kuwa kisanduku hicho hakikuhusishwa na uhalifu wowote na kwamba wanaruhusiwa kuweka pesa hizo. BBC imeenda katika Idara ya Polisi ya New York (NYPD) ili itoe maoni.

"Tumepata visanduku vingi hapo awali," Bw Kane alisema. "Na kisha nikaona idadi ya noti na kufikiria: 'Hii haiwezekani.'

"Tulilitoa nje na ilikuwa ni rundo kubwa la mamia," aliongeza. "Hili ni rundo nene - zimelowa, zimeharibiwa sana."

"Hakukuwa na vitambulisho katika kijisanduku, wala namna ya kumpata mmiliki halisi,," Bi Agostini alisema. "[Polisi] walisema: 'Hongereni!'"

Uvuvi wa sumaku unahusisha kuvuta kamba yenye sumaku kali kupitia maziwa na mito na kuona kile kinachovutwa juu.

Wanandoa hao walisema walianza uvuvi wa sumaku wakati wa janga la Covid-19 na kuongeza kuwa siku za nyuma, wamewahi kupata maguruneti ya zama za Vita vya Pili vya Dunia, bunduki za karne ya kumi na tisa na pikipiki ya kubwa.