Raia wa China wakiri kujihusisha uhalifu wa mtandaoni nchini Zambia

Raia hao wa China wanatazamiwa kuhukumiwa siku ya Ijumaa, vyombo vya habari vya nchini vinaripoti.

Muhtasari

•Wao ni miongoni mwa 77 waliokamatwa Aprili kuhusiana na kile mamlaka ilichoeleza kama "kundi la kisasa la ulaghai kwenye mtandao".

Image: BBC

Raia 22 wa China wamekiri kutenda uhalifu unaohusiana na mtandao nchini Zambia.

Wao ni miongoni mwa washukiwa 77 waliokamatwa mwezi Aprili kuhusiana na kile mamlaka ilichoeleza kama "kundi la kisasa la ulaghai kwenye mtandao".

Kutokea kwa kampuni inayomilikiwa na Wachina katika mji mkuu, Lusaka, kumefuatia ongezeko la kutisha la visa vya ulaghai wa mtandao nchini humo, vinavyolenga watu katika nchi mbalimbali duniani.

Raia hao wa China wanatazamiwa kuhukumiwa siku ya Ijumaa, vyombo vya habari vya nchini vinaripoti.

Kumekuwa na kesi zinazoongezeka za Wazambia kupoteza pesa kutoka kwenye akaunti zao za simu na benki kupitia mipango ya utakatishaji fedha ambayo inaenea hadi nchi nyingine za kigeni, Tume ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DEC) ilisema mwezi Aprili.

Watu katika nchi zikiwemo Singapore, Peru, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na nyinginezo barani Afrika pia wamelengwa katika kashfa hiyo ya mtandaoni, mamlaka ya Zambia ilisema.

Makumi ya vijana wa Zambia pia walikamatwa baada ya kudaiwa kuajiriwa kuwa mawakala wa vituo vya simu katika shughuli za ulaghai, ikiwa ni pamoja na ulaghai wa mtandaoni, DEC ilisema wakati wa ukamataji.

Baada ya kesi iliyodumu kwa wiki kadhaa, raia hao 22 wa China, akiwemo mwanamke mmoja, walikiri mashtaka matatu, uwasilishaji mbaya unaohusiana na kompyuta, uhalifu unaohusiana na utambulisho, na kuendesha mtandao au huduma kinyume cha sheria.

Siku ya Jumanne, mwendesha mashtaka wa serikali aliomba mahakama kujumuisha maelezo zaidi kuhusu mashtaka. Raia hao wa Zambia walishtakiwa mwezi Aprili na kuachiliwa kwa dhamana ili waweze kusaidia mamlaka katika uchunguzi wao.